Saturday, October 8, 2011

DUNIA NZIMA KIJIJINI BUTIAMA LEO.

BUTIAMA.

MABALOZI WATEMBELEA KIJIJINI BUTIAMA.

MABALOZI wanaowakilisha nchi mbalimbali Tanzania Tanzania kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii wametembelea kijiji cha Butiama alipozaliwa mwasisi wa Taifa hii hayati Mwalimu Julius Nyerere ambapo waliongozwa na mwenyeji wao, Waziri wa mambo ya nchi za nje, Bernad Membe.

Mabalozi hao walikaribisha nyumbani kwa Baba wa Taifa jana majira ya saa 8 mchana na mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere, watoto wake, Makongoro Nyerere,Madaraka Nyerere na Emily Magige Nyerere na kupata chakula cha mchana nyumbani kwake kilichoandaliwa na familia hiyo,wakiwemo viongozi wa Mkoa na baadhi ya wananchi wanaoishi kijijini hapo.

Akizungumza katika hafla hiyo mara baada ya kuzulu kaburi la Baba wa Taifa, Mkuu wa mabalozi nchini kutoka Congo, Juma Mpango alisema kumbkumbu ya kifo chake na maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru inawapatia heshima kubwa ya kumuenzi Baba wa Taifa aliyekuwa mstari wa mbele kutetea Amani, Haki, Umoja na Usawa kwa watu wote na kuweka lugha moja nchini ambayo imewangusha watanzania wote.

Aidha amewatakiwa watanzania kote nchini mudumisha Umoja huo ambao ni kuenzi yote mema aliyofanya na kuwatakiwa maadhimisho mema yenye tija ili kudumisha Amani iliyopo nchini Tanzania.

Awali akitoa salamu zake kwa wageni na wanakijiji cha Mwitongo, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa,John haule alisema siku hiyo ni kumbukumbu kubwa kwa Taifa na kijiji cha Butiama kwa wageni kutoka dunia nzima kwani ni haki kuwa Baba wa Taifa alikuwa kielelezo chema kwa nchi zote na barani Afrika na kudhamini kuwa watu wote ni ndugu.

Naye Waziri wa Mambo ya nchi za nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe alisema Wizara yake ameamua kuadhimisha mika 50 ya Uhuru kwa kuwapeleka Mabalozi kutoka nchi mbalimbali na kutembelea vivtio vya utalii katika mbuga ya wanyama ya Serengeti na kujionea maajabu mbalimbali yaliyoko Oldupai Laitol kuona bindamu wa kwanzaaliyeanza kutembea mika Mulioni tatu iliypita na nyayo zake kubakia ambapo zilifukiwa.

"Wataenda kuangalia nyayo za binadamu wa kale ambapo kuna nyayo za mwanamke, mwanaume na mtoto walipita kwenye tope la moto wa volkano na baada ya siku tatu uji ule ulikauka n anyayo zao kubakia nadani walipoendelea mbele walikufa kwani tope hizo ni za moto sana,zikabaki na kufukiwa na mchanga"Alisema Membe.

Akizungumzia wasifu wake alsema Mwalimu Nyerere alikuwa kiumbe wa pekee anyaestahili heshima ya kipekee kwani alikuwa mkombozi kataika kupigamia Uhuru wa nchi yake na nchi zingine, na kwmaba ni viongozi wachache duniani wanaoweza kuiga mfano wake na alisimamia Umoja nchini barani Afrika na kuvunja udini n akuwaunganisha watanzania ambapo mapaka sasa mika 50 ya Uhuru nchi hii haijawahi kupigana wao wao.

Alisema atakumbukwa kw akuunganisha n akuleta mshikamano pia alikuwa mtu mwenye huruma na mpenda dini na hakupenda nchi Tajiri kunyonya nchi masikini na kwmaba kw amatendo hayo mema kwa mwnyezi Mungu Jina lake liko katika mapendekezo atangazwe 'Mtakatifu' na atakuwa hivyo sasa ataitwa Mtakatifu Julius Nyerere.

Kwa kuwa Baba wa Taifa alikuwa rafiki wa Rais Alafat wa Palestina, Balozi wa Palestina ametangaza kumuenzi kwa kuweka jina lake kwenye barabara mojawapo ya Mji wa Lamala kuanzia Novemba mwaka huu.

Akitoa shukrani kwa niaba ya familia nzima, mtoto wake Makongoro Nyerera alisema haiwajawahi kutokea nchini na hata kijiji cha Mwitongo siku ambayo ameona ni kumbukumbu nyingine mpya ambayo itakuwa historia nyingine mpya na kufungua ukurasa mpya wa utalii nchini Tanzania hasa katika kijiji cha Butiama.

Alisema ilikuwa kwao kzai kubwa kuwaomba na kukubali ujio wao imeleta sifa na kuona kuwa kumbe Baba yake alikuwa ni mtu wa waatu wote na kwamba mgeni wa mwisho wa kimataifa kutembelea nyumbani kwao ni Rais Mstaafu wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela.

Akiaga ugeni huo, Mkuu wa Mkoa wa Mara,John Tupa amemwakikishia Waziri Membe kuwa atawaalika mara kwa mara kutembelea vivutio vilivyoko nchini na Mwitongo kwa ujumla.

Nchi zilizokuja ni Angola ,DRC, Belgium, Canada, Dernmark, Finland, ujerumani, India, Italy, Nigeria, Ireland, Namibia, Nertherlands, Nigeria, Norway, Pakistani, Palestina, rwanda, Afrika Kusini, Sweden, Umoja wa falme za kiarabu,Umoja wa Ulaya, Uganda, Zambia, Zimbabwe, Bangladesh, |China, Malawi, Uturuki,Comoro, Marekani, Mashirika ya ADB, UNDP

No comments:

Post a Comment