MUSOMA/SERENGETI.
MBIO za Mwenge wa Uhuru Mkoani Mara zimemaliza vyema kwa kuweka mawe ya MSingi na kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Mtumwa Rashid Khalfani katika Wilaya mbili za Musoma vijijini na Serengeti.
Akisoma risali ya Utii, Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa alisema Mwenge wa Uhuru na Miaka 50 ya Uhuru imefungua nyumba mbili za walimu katika shule ya Sekondari ya Osward Mang’ombe na Jengo la OPD Zahanati ya Masurura za Butiama,Wilaya ya Musoma Vijijini zilizogharimu jumla ya Sh 364,740,500.
Aidha Mwenge wa Uhuru umepitia miradi minne yenye thamani ya Sh. 207,619,980 na Mradi wa Soko la Musati na Ujenzi wa shule ya Msingi Mapinduzi ‘B’na Zahanati ya Park Nyigoti na ofisi ya kijiji cha Robanda ilizinduliwa.
Mwenge wa Uhuru 2010 Wilayani Serengeti ulipitia miradi mitatu hadi kukamilika kwake ilikuwa na thamani ya Sh. 201,516,729.89 na kufunguliwa.
Aidha ujenzi wa nyumba mbili za walimu Shule ya Sekondari Osward Mang’ombe uligharimu jumla ya Sh. 300,000,000 kati ya hizo Mchango wa Mbunge wa jimbo Nimrode Mkono ukiwa ni Sh. 274,000,000.
Ujenzi wa jengo la Zahanati ya Masururla umegharimu kiasi cha Sh. 64,740,500, soko la Musati limegharimu kiasi cha Sh. 35,000,000, ujenzi wa Shule ya Msingi Mapinduzi ‘B’ Sh. 75,000,000,Zahanati ya Park Nyigoti ambayo ni guvu kazi ya wananchi wenyewe kupitia ruzuku kutoka halmashauri ni Sh. 34,955,980 na Ujenzi wa ofisi ya Kijiji cha Robana umegharimu Sh.62,664,000 zikiwa ni nguvu kazi.
Alisema kuwa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru 2010 umeendelea kutekelezwa kwa mapambano dhidi ya Malaria na kwamba maambukizi ya malaria yamepungua toka asilimia 49 mwaka 2009/2010 hadi Asilimia 35 mwaka 2010/2011 Wilaya ya Musoma.
Wilaya ya Serengeti maambukizi ya Malaria yamepungua toka 48.9 asilimia sawa na watu 24,496 mwaka 2009/2010 hadi asilimia 27 sawa na watu 50,818 mwaka 2010/2011 na kusababisha kupungua kwa vifo toka 137 kwa mwaka 2009/2010 hadi vifo 97 mwaka 2010/2011.
Wilaya ya Musoma vifo pia vimepungua kutokana na malaria toka vifo 59 mwaka 2009/2010 hadi vifo 42 mwaka 2010/2011, jtihada za makusudi zinahitaji kwani bado muamko wa kutumia vyandarua kwa baadhi ya wanannachi ni changamoto kubwa ambayo inahitaji kutiliwa pamoja na kwamba serikali imetoa vyandarua vyenye dawa(viuatilifu) 154,591 na Wilaya ya Serengeti vyandarua 115,816.
Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru umezinduliwa Mkoa wa Mara kijiji cha Mwitongo, Butiama mahali alipozaliwa Baba wa Taifa hili Hayati Mwalimu Julius Nyerere na maadhimisho ya miaka 12 tangu kifo chake ambapo mara baada ya kuwashwa kwa Mwenge wa Uhuru na Makamu wa Rais, Dk Mohammed Bilal na Mwenge wa Mwitongo,Mvua kubwa ya ghafla ilinyesha.
No comments:
Post a Comment