YAFUATAYO NI MASWALI YA KUMUULIZA MAMA MARIA NYERERE:
1-Oktoba 14 mwaka huu, Tanzania itaadhimisha miaka 12 tangu kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Unapenda kuwaeleza nini
Watanzania kuhusu siku hii.
2- Unadhani inatosha kwa watanzania kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuwasha mwenge Butiama ama kuandaa makongamano?
3- Binafsi unayaonaje maisha bila ya kuwa na Mwalimu Nyerere?
4- Ni changamoto zipi ulizowahi kukumbana nazo ukiwa mke wa rais?
5-Unadhani ni kwa nini Mwalimu Nyerere aliwalea watoto wake sawa na watoto wengine wa Kitanzania wakati ambapo
kwa madaraka aliyokuwa nayo, angeweza kuwapeleka nje kusoma ama wangeishi kifahari sana?
6-Ni kwa nini Mwalimu Nyerere hakujihusisha kabisa na biashara ama kujilimbikizia mali katika kipindi chote
alichokuwa madarakani hadi alipostaafu urais?
7- Ni kwa nini wewe binafsi katika kipindi chote cha uongozi wa Mwalimu Nyerere hukutaka kuanzisha taasisi ya mke wa
rais kama ilivyo kwa wake wengine wa marais duniani?
8- Ni kitu gani kilichowahi kumchukiza sana Mwalimu Nyerere katika maisha yake?
9-Na ni kipi ambacho kiliwahi kumfurahisha, iwe akiwa madarakani au hata baada ya kustaafu?
10-Wewe binafsi ni tukio lipi, ambalo liliwahi kukuhuzunisha katika maisha yako? Na tukio lipi liliwahi kukufurahisha?
11-Tanzania inaelekea kutimiza miaka 50 ya uhuru. Wapo wanasiasa wanaobeza kwamba hakuna chochote
kilichofanyika kuiletea nchi maendeleo. Unasemaje kuhusu kauli hizi?
12- Una maoni gani kuhusu siasa ya vyama vingi hapa nchini? Unadhani vinaisaidia serikali katika kuendesha mambo yake
ama vinaweza kuhatarisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa watanzania?
13- Nini maoni yano kuhusu matukio ya vurugu, ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara wakati wa chaguzi
ndogo za ubunge na udiwani?
14- Tanzania imetoa wanawake wengi katika ngazi za uongozi, kitaifa na kimataifa. Unadhani wakati wa Tanzania kuwa
na rais mwanamke umewadia?
15- Unatoa mwito gani kwa wanawake wa Tanzania, hasa wale waliojitosa katika masuala ya siasa ama kupewa
nafasi za juu za uongozi?
No comments:
Post a Comment