Thursday, May 31, 2012

MTOTO AKITOKA KUNYWESHA NG'OMBE LAMBO TARIME


SAKATA LA KUMKATAA DC TARIME LAGONGA MWAMBA

SAKATA LA KUMKATAA  DC TARIME LAGONGA MWAMBA
TARIME.

SAKATA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Tarime Mkoani Mara la
kumkataa na kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete kumwondoa Ukuu wa Wilaya,
Mkuu wa Wilaya John Henjewele limeingia sura mpya baada ya madiwani
kugawanyika wengine wakitaka aondolewe na huku wengine wakiomba  apewe
muda wa kujibu tuhuma zinazomkabili.



Licha ya kuwa kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichopita Mei 08
2012 madiwani wa CCM pamoja na wa kambi ya upinzani waliungana pamoja
kujenga hoja ya kutaka Henjewele kuondolewaTarime,kwenye kikao
kilichofanyika Mei 30 ambapo baada ya  hoja hiyo kugusiwa na madiwani
toka kambi ya upinzani iliwagawa madiwani ambapo madiwani toka CCM
waliwageuka wale wa Chadema.



Kwa hali hiyo Madiwani wakambi ya upinzani walijikuta wanaingia wakati
mugumu walipojaribu kukumbushia msimamo wao wa maazimio ya kikao
kilichopita ambapo madiwani wote kwa pamoja walikuwa na kauli moja ya
kumkataa Henjewele,CHADEMA walijikuta CCM wanawageuka kwa madai kuwa
hoja hiyo haikuja  kwa wakati mwafaka.



Kufuatia utata huo ambao ulisababisha kikao kuonyesha hali ya
kutokalika na  malumbano ya kwa baadhi ya  madiwani hasa wa kambi ya
upinzani huku wakitishia kususia kikao na kujigeuza kuwa kamati hali
ambayo ilimlazimu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Fidelis Lumato
kusoma kanuni namba 17 yenye kumpat fursa Mwenyekiti kumwondoa Diwani
yeyote  anaye leta fujo ndani ya kikao kwa  kumtaja kwa jina ili
achukuliwe hatua ikiwa ni pamoja na kutolewa nje ya kikao na
kutohudhuria vikao vitatu mfululizo katika baraza hilo, hali iliyo
leta utulivu nakuendelea na kikao.



Sagara alilazimika kuwa mkali baada ya kanuni kusomwa kuwa anaye kiuka
utaratibu na kuvuruga kikao lazima awajibishwe kwa mjibu wa kanuni
ambapo sagara alitishia madiwani mawili toka kambi ya upinzani kutoka
nje ya kikao kwa kuwa wanaonekana kuvuruga kikao baada ya hapo Diwani
Mang'enyi Ryoba  toka kata ya Nyanungu(Chadema)  kuwatetea wenzake
kuwa awasamehe ilikuendelea na kikao na kwamba ni changamoto kwao,
ambapo Mwenyekiti aliridhia ombi hilo na kuwasamehe ili kuendelea na
kikao.



Aidha kwa kuhitimisha mjadala huo ulioleta utata huku baadhi ya
madiwani toka kambi ya upinzani wakisimama bila ruksa ya Mwenyekiti
midhili ya nyumbu, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Amosi Sagara
aliwataka Madiwani kufuata utaratibu kwa kuunda kamati itakayo kwenda
kwa  Mkuu wa Mkoa John Tuppa ili wapate  majibu kuhusiana na maazimio
ya kikao kilicho pita .

Awali Madiwani hao waligomea kikao kilichopita kwa   kumtuhumu Mkuu wa
wilaya John Henjewele kuwa ameshindwa kuondoa kizuizi cha polisi
kilichopo kijiji cha  Magena kwa madai kuwa hakina msaada wowote na
wananchi.

kikao hicho kilihusu ripoti ya ukaguzi wa hesabu za Serikali na
kupitia miradi ya mwaka wa fedha ya mwaka 2010/2011.

HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME YATAKIWA KUONGEZA VYANZO VYA MAPATO



HALMASHAURI ya Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara, imetakiwa kuongeza vyanzo vyake vya mapato ili iweze kujitosheleza yenyewe katika sehemu kubwa ya matumizi si ya kutegemea ruzuku toka serikalini.

Akiwasilisha taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu taarifa ya fedha za halmashauri ya Wilaya ya Tarime kwa mwaka wa fedha uliouishia Juni 30 2011 Mkaguzi Mkazi Msaidizi Mkoa wa Mara, Deogratius Waijaha alisema kuwa asilimia 91.4 ya halmshauri inategemea ruzuku kuu, hivyo lazima ianzishe na kubuni mipango ya kuifanya ijitegemee na sio kutegemea ruzuku kutoka Serikali kuu.

Waijaha alisema kuwa mapato ya ndani ambayo ni Sh. Bilioni 1,503,489,981 ni madogo sana ukilinganisha na ruzuku inayopewa halmashauri kutoka Serikali kuu ya kiasi cha Sh. Bilioni 20, 960, 601,198.

Kwa upande wa matumizi ya kawaida alisema kuwa halmashauri ilitumia kiasi ch Sh. 17,604,608,018 kwa matumizi ya kawaida wakati ambapo mapato yake ya kawaida  yalikuwa Sh. Bilioni 18,238,072,617 ikionyesha kwamba kulikuwa na Balance ya Sh. 633, 464,599.

Mkaguzi huyo alisema kuwa kwa mwaka wa fedha 2010/2011 halmashauri ilikusanya Jumla ya Sh. 1,503,489,981 kutoka katika vyanzo vyake ukilinganisha na bajeti yake ya Sh. 1,263,405,000 na kusababisha makusanyo zaidi ya Sh. 240,084,981 yakiwa sawa na asilimia 19.

Maeneo ya faini na tozo yalibajetiwa kukusanya kiasi cha Sh. 583,405,00 lakini kiasi kilichokusanya  kilikuwa Sh. 549,769, 083 ikiwa na upungufu wa Sh. 33,635,  916 sawa na 5.8 ambapo kodi ya ndani ilibajetiwa kiasi cha Sh. 680,000,000 lakini kiasi kilichokusanywa kilikuwa na Sh. 868,036,449  ikiwa ni ongezeko zaidi ya Sh. 188, 036,449 ikiwa ni sawa na asilimia 27.7


Mkaguzi Waijaha alisema kuwa halmashauri imepata hati inayoridhisha ambapo aliipongeza kwa kusimamia vyema rasilimali na fedha za halmashauri na kwamba hali ya fedha ya halmashauri hadi Juni 30 2011 na kwamba matokeo ya utendaji na mapato halisi kwa mwaka ulioishia inawiana na viwango vya kimataifa vya uandaaji wa hesabu za fedha kwa sekta ya Umma.


Pia alisema katika manunuzi yenye jumla ya Sh. 32,050,000 yaliyokusanywa kupitia programu ya maendeleo ya kilimo (ASDP) yalikiuka kanuni Na. 49 ya manunuzi ya umma ya mwaka 2005 kwa kununua vifaa huska katika kiasi kidogo kidogo kupitia hati mbalimbali za malipo badala ya kufuata taratibu za Zabuni kama ilivyokuwa ikihitajika na kanuni husika.

Tuesday, May 29, 2012

WANANCHI WATAKIWA KUJUA SHERIA YA PAROLE


MUSOMA

WANANCHI wa Mkoa wa Mara, wametakiwa kufahamu utaratibu wa kisheria wa wafugwa wenye kifungo kirefu wanaoonyesha mwenendo mzuri wa kurekebika wawapo Magereza (PAROLE), na kumaliza kifungo chao wakiwa  nje  ya gereza na si kuwakataa.


Hayo yalisemwa Mei 29 Mwaka huu katika uzinduzi wa Bodi ya Parole, Afisa Mwandamizi Afisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Buhacha Kichinda alipokuwa anazindua bodi hiyo yenye jukumu la kupitia majalada ya wafugwa wenye nidhamu wawapo katika vifungo vyao magerezani.

Alisema hiyo ni changamoto kubwa inayowakabili wafugwa wanaoachiwa kwa sheria ya Parole kukataliwa na wananchi wanapotakiwa kumalizia kifungo chao wakiwa majumbani mwao, jambo ambalo lilikuwa kikwazo kwa utekelezaji wa sheria hiyo.


Aliongeza kuwa elimu inahitaji kwa wananchi juu ya umuhimu wa Parole kwa kushirikiana na viongozi wa Serikali ili wananchi waweze kushirikiana nao kwani wamekuwa tayari wamehakikiwa kuwa wana tabia hivyo na wengi  kujishughulisha katika majukumu mbalimbali ya ujenzi wa Taifa kwa kujishughulisha na kilimo, ufugaji, uvuvi na  biashara ndogo ndogo.


Ameitaka bodi hiyo kufanya kazi za uchunguzi wa majalada kwa kina ili wafugwa hao wanapokuwa na kifungo cha nje wasifanye uhalifu tena na kusababisha kutoaminiwa kwa bodi.


Awali akisoma taarifa ya Parole, Mkuu wa Magereza  Mkoa (RPO), Melchadus Mwendwa alisema kuwa ofisi yake imekuwa na changamoto mbalimbali za kufuatilia taarifa muhimu za kukamilisha majalada ya wafugwa wanaopekezwa kuachiliwa ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa nakala za hukumu toka Mahakamani,taarifa za uhalifu za awali toka jeshi la polisi,ufinyu wa bajeti na uelewa mdogo wa Sheria ya Parole kwa viongozi wa vijiji/mitaa anapochagua kuishi mfugwa.

Alisema kuwa kati ya wafugwa 268  wafugwa 10 tu waliovunja masharti wengi wao wakitenda makosa mengine ya jinai na kuwalazimu kurudishwa gerezani kwa mujibu wa sheria na  wafugwa wapatao 40 wakiendelea na vifungo vyao chini ya utaratibu wa Parole wakiwa katika mitaa na vijiji walipochagua kuishi  na wafugwa wapatao 219 tayari wamemaliza vifungo vyao chini ya utaratibu huo.

Sheria ya Bodi ya Parole N0. 25/1994 na marekebisho yake No. 5/2002, kanuni za bodi ya Parole No. GN 563/1997 vilianza kutumika mwaka 1999 na kwa mujibu wa kifungu cha 3(3) cha Sheria ya Bodi za Parole kinaidhinisha ziundwe Bodi za Parole Mikoa ambayo kwa Mkoa wa Mara zilizinduliwa Mei 29 ambayo kazi  zake ni kupitia kila jalada la mfugwa lenye vielelezo vinavyojitajika toka sehemu mbalimbali, aliyependekezwa kuachiliwa kwa Parole na kuthibitisha viwango vya sifa za mfugwa ili akubalike.


Aidha kati ya majalada ya wafugwa wapatao 321 yaliyopekezwa na Bodi ya Parole Mkoa wa Mara tangu utaratibu huo uanzishwe ni majalada 22 tu ambayo bado yapo kwenye Bodi ya Parole Taifa yanayofanyiwa mchakato wa kuyapeleka kwa Waziri huska ili ayatolee uamuzi  idadi ambayo hairidhishi.

Wednesday, May 23, 2012

DC TARIME ADAIWA KULIDHALALISHA KANISA

Dinna Maningo, Tarime.
MCHUNGAJI wa Kanisa la Pentecostal Evangelistic Fellowship Africa(PEFA) Tawi la Gonsarara Kijiji cha Kewanja Kata ya Kemambo-Nyamongo Wilayani Tarime Elia Magutu amewataka viongozi wa Serikali kutumia hekima na kauli za busara pindi wanapohutubia wananchi kupitia mikutano ya hadhara.
Kauli hiyo imekuja baada ya mchungaji  Magutu kudai kuwa  hivi karibuni May 3 Mkuu wa Wilaya John Henjewele akiwa anahutubia wananchi wa kitongoji cha Gonsarara kijiji cha Kewanja alidaiwa kulikashifu kanisa na kusema kuwa kanisa la PEFA halipo kihalali bali limeibuka na kuanzishwa kwa lengo la kufanyiwa tathimini ya malipo katika zoezi  linaloendeshwa na mgodi wa Dhahabu wa North Mara unaoendelea na tathimini kwa ajili ya kuwahamisha wananchi wanaoishi jirani na mgodi wa dhahabu kitongoji cha Gonsarara.
“Ilikuwa tarehe   3 May Mkuu wa Wilaya Henjewele akiwa katika mkutano wa hadhara Gonsarara akiwa anazungumzia tathimini alisema kuwa kuna watu wamekuja kutoka Mwanza  na kujenga  nyumba  ili nao wafanyiwe tathimini na mgodi wakati anaendelea na maongezi alisema kuna Kanisa limeibuka la kitapeli lisilojulikana na limetegeshwa ili nalo lifanyiwe tathimini ya malipo kauli hiyo ilitushangaza kwa sababu katika hicho kitongoji kuna kanisa moja tu ambalo ni kanisa la PEFA  moja kwa moja ndilo alilokuwa analilenga”alisema Magutu.
Mchungaji Magutu alikanusha madai ya Mkuu wa Wilaya Henjewele la kuibuka kwa kanisa ambapo alisema kwa kuonyesha vielelezo mbalimbali kuwa kanisa hilo lipo kwa muda mlefu tangu mwaka 1996 na kwamba kauli hiyo ni kulizalalisha kanisa.
“Hili kanisa halijajengwa leo limeanzishwa toka mwaka 1996 wakati huo tukiwa tunasali shuleni Nyabigena-Kewanja ilipofika mwaka 2002 tukanunua eneo Gonsarara tukajenga nyumba ya nyasi kulingana na uwezo mdogo tuliokuwa nao wakati huo tukaendelea kusali likiwa linaongozwa na mzee wa kanisa aitwae Dishon Ghati baadae tukajenga nyumba ya bati na sasa tunaendelea na ukarabati na kanisa ambalo hadi sasa lina zaidi ya waumini 100”alisema Mchungaji.
Mchungaji huyo alisema kuwa amesikitishwa na kauli hiyo ya Dc Henjewele na kumtaka aliombe radhi kanisa kwa madai kuwa amelidhalalisha na kulikasfu hadharani bila kujua kwa undani historia ya kanisa hilo la PEFA.
“Kama Dc alikuwa na mashaka na kanisa alipaswa afike kanisani aonane na uongozi wa kanisa tumweleze historia ya kanisa siyo kuongea hadhalani kitu asichokijua,kanisa lipo kwenye eneo halali tunamuomba achunguze kwa undani zaidi na hatuna sababu yoyote ya kuhamishwa na wala hatujaomba mgodi utuamishe kama mgodi umeona kanisa lipo jirani na mgodi na kunahaja ya kuamishwa kwa shuguli zao ni maamuzi yao wenyewe”alisema
Aliongeza” Sisis hatuna taarifa yoyote wala barua kuwa mgodi unataka kufanya tathimini kanisa na kuliamisha na itambulike kuwa kanisa la PEFA  ni taasisi inayotambulika lina haki ya kujiendesha kikanisa,kuboreshwa kwa kanisa  Dc anasema tunafanya  hivyo kwa ajili ya malipo ya kuhamishwa! Je toka tathimini imeanza ni kanisa lipi ambalo limefanyiwa tathimini? Hakuna.
Mchungaji Magutu alisema kuwa kutokana na kauli ya Dc Henjewele huwenda ikaathili waumini  kwa kudhani kuwa halikuwa kanisa bali lipo kwa ajili ya kutafuta masalahi binafsi ambapo pia aliwataka waumini kuendelea kusali na kumtumikia Mungu nakwamba wasikatishwe tamaa na  kauli ya Henjewele.
Mwenyekiti wa kanisa la PEFA Wilaya ya Mashariki Tarime Mchungaji Samson Msabi alithibitisha kuwepo kwa uhalali wa kanisa hilo ambapo alisema aliliweka wakfu mwaka 2008.
Pia Mwenyekiti wa Kijiji cha Kewanja ambako ndiko kuliko na kanisa hilo Tanzania Omtima( Chadema) alithibitisha kuwepo kwa kanisa ambapo alisema analitambua kutokana na kuwepo kijijini kwake kwa muda mlefu.
Mkuu Wa Wilaya ya Tarime John Henjewele alipoelezwa tuhuma hizo dhidi yake alikili kuwepo kwa kanisa hilo nakusema siyo  kanisa halali nakwamba limeibuka na kutegeshwa kwa lengo la kufanyiwa tathimini na mgodi na kwamba ameliona hilo kanisa kwa macho yake ambalo alisema halijui jina la kanisa kwakuwa kanisa hilo halijaandikwa jina.

MADIWANI WAWASHIKIA WATENDAJI


 RORYA.


MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Mkoani Mara wamemtuhumu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Rorya, Daniel Chacha kutumia fedha vibaya zinazotolewa na Halmashauri kwenda katika vituo vinavyotoa huduma ya afya kwa ajili ya kununua vifaa,dawa na mahitaji mengine huku akidaiwa kutofikisha baadhi ya vifaa kwenye vituo.

Hayo yalibainishwa katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika jana ambapo Madiwani walisema kuwa kuna baadhi ya wakuu wa idara wamekuwa wakitumia vibaya fedha za Serikali ambapo walisema kuwa kuna fedha ambazo zilitolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo lakini hazitumiki ipasavyo.

Diwani wa kata ya Kyango’mbe Emanuel Manyama,(Matongwe) CCM alisema kuwa kuna kiasi cha fedha Milioni 20 zilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Bitiryo lakini fedha zilizoingizwa kwenye akaunti si kiwango  kamili kilichotolewa na Halmashauri.

“Kuna ndume tatu ambazo ni tatizo kwenye Halmashauri DMO,DT na Mhandisi wa maji hawa watu ni wala fedha kijiji cha Bitiryo zilitengwa  Milioni 20  kwa ajili ya ujenzi cha kushangaza fedha zilizoingizwa kwenye akaunti ya kijiji ni Milioni 17 tu Milioni 3 hazionekani  zimebaki Halmashauri lakini hapa kwenye kablasha naambiwa milioni 20 ziliingizwa kwenye akaunti ya kijiji na zimetumika kujenga zahanati na wakati ni Milioni 17 zilizowekwa kwenye akaunti naomba nielezwe hizo pesa zingine zimekwenda wapi na kwanini hazikuwekwa kwenye akaunti”alisema Manyama.

Diwani wa viti maalumu Tarafa ya Nyancha Pendo Odero CCM  aliongeza kwa kusema kuwa Mganga mkuu Chacha anatuhumiwa kwa kutofikisha fedha za vifaa na dawa kwenye baadhi ya vituo vya afya nakwamba baada ya kufahamu tuhuma hizo alianza kuwahamasisha wanafunzi kumfichia siri ya kutofika kwa fedha za vifaa.

“DMO kala pesa za Halmashauri za kununua vifaa na hata dawa zilizotolewa kusambazwa vituoni hazijafika baada ya yeye kugundua mambo yameharibika alichukuwa gari kwenda kuwahamasisha watumishi na kuwadanganya waseme pesa na vifaa vimefika lakini mipango yake ikavunjika akiwa safarini taarifa zikafika kwa mkurugenzi na Mwenyekiti wa Halimashauri wakazyuia gari na kumtaka astishe zoezi hilo”alisema Odero.

Diwani wa kata ya Mirare Peter Ayoyi( CCM),alilalamikia Madiwani kutopatiwa vitambulisho vya Bima ya afya  licha ya kuwa tayali walishatoa fedha za malipo ya vitambulisho.

“DMO atueleze hatima ya vitambulisho vyetu vya bima ya afya Madiwani tumeshalipa pesa 3,000 kwa kila Diwani ambapo 3,000 zingine kwa kila Diwani,  Halmashauri inachangia jumla kila Diwani ni 6,000 tumetoa lakini hatujaletewa vitambulisho na hivi karibuni nimeenda Bima ya afya Mwanza wakasema hawajapokea fedha za Madiwani kutoka Rorya DMO tuambie pesa zetu umezipeleka wapi.”alisema Ayoyi.

Hata hivyo Mganga Mkuu Daniel Chacha alikwepa kujibu baadhi ya maswali huku maswali mengine aliyojibu kudaiwa kutowaridhisha Madiwani ambapo kwa upande wa vitambulisho vya Bima ya afya  alisema kuwa vitambulisho vimekataliwa kwa madai kuwa hakuna mchango wowote uliowasilishwa  kwa ajili ya kupatiwa huduma hiyo ya vitambulisho.

Madiwani hao hawakuishia kwa Mganga Mkuu pia walimvaa Mweka Hazina wa Halmashauri,Caiser Ninalwo  na kumtuhumu kushindwa kusimamia fedha zikiwamo asilimia 20 inayotolewa na Halmashauri kwenda katika vijiji ambapo walimlalamika kuwa kumekuwa na upungufu wa fedha zinazotolewa kwenda kwenye vijiji huku vijiji vingine vikidaiwa kutofikiwa na fedha .

“Miongoni mwa Madiwani waliolalamika  kutolewa kwa fedha kidogo kwenye vijiji ni Diwani wa kata ya Ikoma Laurent Adriano (CCM) Diwani wa kata ya Koryo Peter Sarungi (CCM) Diwani kata ya Kitembe Thomas Patrick( Chadema) Diwani wa kata ya Kigunga Magesa Magige (CCM).

“Kuna fedha inayotolewa na Halmashauri asilimia 20 kwenda kwenye vijiji lakini kila kwaka fedha zinapungua vijiji 80 vinatakiwa kupa asilimia hiyo mwaka juzi zilitolewa Sh. 613000,mwaka jana zikatolewa tena Sh.430,000, ambapo mwaka huu zimetolewa Sh. 100,000, kiasi hicho ni kidogo hasa ukizingatia serikali imetupatia ruzuku ya zaidi ya Milioni 300 na  kuna vijiji vina akaunti havikuingiziwa fedha  na kuna vijiji havina akaunti fedha zinakwenda wapi?alihoji Sarungi.

Madiwani hao waliomba kupatiwa Nyaraka za fedha zinazotolewa ili kujua na kuthibitisha  kiasi cha fedha zinazokwenda kwenye vijiji kila mwaka mbapo hata hivyo Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Rorya Andreas Madundo alikubali ombi lao na kukubali kutoa nyaraka za fedha zinazotolewa kwa manufaa ya vijiji.

Wakati huo huo madiwani hao wa halmashauri wamemlalamika Mhandishi wa Maji Emmanuel Masanja kwa kutokamika kwa visam vya majia ambpo walisema kuwa kuna fedha zilizotumika katika uchimbaji wa visima lakini hadi sasa visima hivyo havitoi maji.

Naye Diwani wa kata ya kisumwa, Amwolo  Malaki  (NCCR) alisema kuwa jumla ya Sh. Milioni 80 zilitolewa kufufua mradi wa maji katika kijiji cha Malasibora na Nyanchabakenye na kwamba fedha za ujenzi huo zimepotea bila kuwa na manufaa.

“Visima havitoi maji na mashine ni mbovu haifanyi kazi na mkandarasi alipewa Milioni 40 lakini hakuna kisima ambapo kimeishakamilika na ikatangazwa zabuni kwa mkandarasi mwingine na yeye akapewa Milioni 40  akanunua mashine ambayo nayo haikufanya kazi, fedha zimekwisha na hatujui fedha zingine tutapata wapi, wananchi wanaendelea kupata kero ya maji” Alisema Malaki.

Aliongeza “Zaidi ya mika mitatu an nusu maji hayapatikani kamati zmeudwa kufatia lakini hatua zozote zilizochukuliwa madiwani wenzangu kwa machafu haya na kwa kuzingatia kanuni naomba mniunge mkono baraza lijeuke kuwa kamati tuwajadili hawa watu DMO, DT, na Mhandishi wa Maji tumechoka na utendaji wao mbovu kwani kila baraza tunazungumzia mambo yale yale yasiyotekelezwa?Alisema.

Hata hivyo kutokana na majibu yaliyotolewa na wakuu hao wa Idara hizo tatu hayakuweza kuwaridhisha madiwani hali iliyolazimu baraza hilo kugeuka na kukwa kamati ili kuwajadili kwa kina.

Monday, May 21, 2012

SIASA CHAFU ZAANZA WILAYA YA RORYA


Watangaza nia ya Uenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya wameaanza kutumia mbinu za kuhujumiana wao kwa wao huku wakitumia baadhi ya vyombo vya habari kuchafuana.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii ofisini kwake, Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Rorya Samueli kiboye alisema kuwa mmoja ya mgombea ambaye hakutaka kutaja kutaja jina lake alisema ameanza kutumia vibaya vyombo vy ahabari kwa kukiuka taalumu hiyo.

Alisema kuwa kuna moja ya gazeti la kila siku si  Uhuru,limetoa habari kuwa amemkatisha masomo mwanafunzi na kumfanyisha kazi za nyumbani, huku binti huyo akinusha habari hizo kuwa yeye aliamua kuondoka nyumbani kwao kutokana vipigo vya mara kwa mara kutoka kwa Baba Mzazi kumkatisha masomo na  kumlazimsha  kuolewa na ndipo binti huyo alipoamua kutafuta kazi za nyumbani.

“Baada ya Mama yangu mzazi, Wankuru Joseph kufarikia Mwaka 2008,nilibahatika kuchaguliwa na kujiunga na Shule ya Sekondari Nyandoto-Tarime kidato cha kwanza mwaka 2009, hadi cha Tatu sikuwahi kulipiwa ada na mzazi, walimu wakamwandikia barua ya kumtaka alipe ada na wito wa kumwita shuleni lakini hakufanya hivyo, nikafukuzwa shuleni na akaniambia kuolewa nilipokataa alinipiga sana na Kunifukuza alisema Angelina.

Aliongeza kuwa baada ya kufukuzwa na baba yake alitafuta sehemu ya kuishi na kumpata msamalia mwenye ambaye ni Mke wa Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya na kumwambia matatizo yake na kuamua kuishi hapa hadi sasa.

Alisema kuwa hiyo ni hujuma kutoka na watangaza nia wenzake kudurufu ( Photocopy) kwa habari iliyotolewa na kuisambaza katika vijiji ili wananchi waisome kwa nia kum dhoofisha kisiasa.

Aidha amewataka waandishi wa habari kutumia taaluma yao ya kuandika habari sahihi na kwamba wasitumike kwa lengo la masilahi ya mtu binafsi.

Fomu za  kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwa ngazi ya Wilaya na Mkoa zitaanza kuchukuliwa Juni 2 Mwaka huu, ambapo mpaka sasa miongoni mwa wagombea wa kiti cha Uenyekiti Wilaya ya Rorya ni Samuel  kiboye (Namba tatu), Razaro Akuku, Jamoko Kateti na Yoda Ambonya.

Wednesday, May 16, 2012

WAKUU WA WILAYA WAAPISHWA,SMG 3 NA RISASI 430 ZAKAMATA




WAKUU wapya wa Wilaya Mkoa wa Mara jana waliapishwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa tayari kwa kuanza kazi, iliyofanyika katika Ukumbi wa Uwekezaji wa Mkoa wa Mara, uliopo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa.


 Baada ya kuapishwa kwa Wakuu hao wapya wa Wilaya kwa pamoja walikwenda katika ofisi za CCM Mkoa kuweka saini katika kitabu cha wageni jambo ambalo ni mara ya kwanza kufanya hivyo,tofauti na awali kwa kwenda kila mmoja kwa muda wake na siku tofauti.

Shamra  Shamra za kuwaapisha Wakuu hao wapya zilitia fola, kwa wananchi na viongozi mbalimbali waliofurika katika ukumbi huo, jambo ambalo pia liliwashangaza baadhi ya viongozi na kwamba halijawahi kutokea.

Sherehe hizo zilianza kwa dua kutoka katika viongozi wa madhehebu ya dini ya kiislamu na kikrsito ambapo Shehe Mkuu wa Waisalamu Mkoa Shehe Magehe aliomba dua, akifuatiwa na Askofu Mkuu wa  Wakatoliki, Mhashamu Msonganzila.

Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka Wakuu hao wa Wilaya kuwajibika  kwa kufanya kazi kwa uadilifu, uchapa kazi, kuwa na moyo wa kujituma, maono na kuacha alama kama kumbukumbu zao waachapo madaraka na kuwahudumia wananchi  ipasavyo kwani Rais Jakaya Kikwete amewaamini wao.

Alisema kuwa kuna changamoto zinaukabilia Mkoa wa Mara hasa kwa ulinzi na usalama japokuwa bado kuna matukio yanayofanyika lakini yanadhibitiwa haraka.

Alisema kuwa kuna baadhi ya watu kutoka mikoa na Wilaya zinazopakana na nchi jirani wanaingia katika Mkoa wakiwa na silaha na risasi ambapo jumla ya risasi zipatazo 430 na SMG tatu zilikamatwa katika Wilaya za Tarime na Serengeti na kubaini watuhumiwa hao ni wakazi wa Kigoma.

Alizitaja changamoto zingine zinazoukabili Mkoa wa Mara, pamoja na kuwa na rasilimali za kutosha wananchi wake bado ni masikini ambapo Mkoa huku chini ya kiwango cha kitaifa,   kuvushwa  kwa magendo katika Wilaya ya Tarime kwenda nchi jirani ya Kenya na ajira kwa vijana.


“ Kuhusu ajira wapo vijana  ambao hawataki kujishughulisha na huwa vijiwe  asubuhi , hii ni changamoto kubwa, huku kukiwa na fursa nyingi za Mkoa kwa wao kujishughulisha, kuwepo wazi kwa maeneo ya kilimo, huku ardhi ikiwa na rutuba ya kutosha” Alisema Tuppa.


Aliwataka Wakuu hao wapya kushughulikia changamoto hizo kwa pamoja kwa kushirikiana na wadua mbalimbali wa maendeleo wa Mkoa wa Mara.

Walioapishwa majina yao na sehemu zao za kazi zikiwa kwenye mabano ni ni Joshua Chacha Mirumbe(Bunda), Angelina Mabula (Butiama), Jackson Msome( Musoma), Alias Goroe( Rorya), Capt. Mstaafu James Yamungu (Serengeti) na John Henjewele( Tarime).



Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa walihudhuria sherehe hizo wakiwemo pia viongozi wa vyama vingine vya siasa.

VIONGOZI WA VITONGOJI, TARAFA NA KATA WAPATA MSASA



VIONGOZI wa Tarafa,Kata vijijiji na Vitongoji wa Wilaya ya Rorya wamepata Mafunzo juu ya Utawala Bora na uwajibika , ulinzi shirikishi na rushwa katika eneo lao la kazi.

Akitoa mafunzo hayo ya siku mbili yaliyofanyika katika kijiji cha Sudi Tarafa ya Mirare Wilayani humo, Afisa Utumishi wa Wilaya hiyo, Sebastian Masanja  aliwataka viongozi hao kuwatumikia wananchi wao na kuhakikisha wanatoa taarifa za mapato na matumizi kwa wananchi kwenye mikutano mikuu ya vijiji WDC na taarifa zote na michango ya wananchi,tozo, wahisani,Halmashauri na Serikali kuu.

Alisema kuwa upo udhaifu wa kutofanya vikao ambao unasababisha kuwepo kwa ugomvi hasa wa ardhi na kutokusanya ushuru kwa maduka na migahawa iliyopo katika vijiji hivyo.

Aliwataka viongozi hao kuweka utaratibu wa kuwajibishana kati ya viongozi wa kuchaguliwa na wananchi pamoja na watumishi wa Umma.

Aidha aliwataka viongozi hao kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwa na mashamba ya mfano, miradi midogo midogo ya kuwawezesha kujikimu katika familia zao kama ufugaji wa kuku, bata na mbuzi ili wananchi waige mfano wao, kwani kwa kufnaya hivyo itawasababisha kuondokana na umasikini.
Pia amewahimiza kuachana na mila potofu ya kuridhi wajane kwani kwa kufanya hivyo ni kuongeza ongezeko la waathirika wengi wa Ugonjwa wa Ukimwi ukizingatia kuwa Wilaya ya Rorya ndiyo yenye maambukizi makubwa kiwilaya.

Aidha aliwataka kusaidia kampeni mbalimbali za kitaifa mfao, kupima VVU, chanjo za watoto, panga uzazi, kuwa na choo bora, kuchemsha maji ya kunywa, kunawa mikono kwa sabuni, kuwa waaminifu katika mapenzi na kuacha vitenndo vya uzinzi, kujitolea kwenye shughuli za maendeleo, kuvaa mavazi yenye heshima, kuazisha vikundi yva ulinzi shirikishi jamii na kupiga vita rushwa.

Akitoa mada juu ya ulinzi shirikishi,Mkaguzi Msaidizi wa jeshi la polisi, Antony kahema aliwataka viongozi hao kuacha tabia ya kujichukuliwa mamlaka na kuwanyanyasa wananchi kwa mamlaka waliyopewa na badala yake wawafikishe katika mikono ya sheria.

“Nashangaa wapo baadhi ya watendaji wa kata na vitongoji na vijiji wamekuwa wakiwanyanyasa wanachi aidha kwa kuwapiga na kuwafungia masaa 24 katika ofisi zao wale wanaosaidikiwa kuwa na tuhuma, hili ni kosa kwani kazi yenu ni kuwasiliana na jeshi letu ili hatua za kisheria zichukuliwe na si kuwapiga hadi kusababisha maumivu makali.”Alisema Mahema.

Aliwataka kuwa na utii wa sheria pasipo kuwa na shuruti na si kiongozi kuhamasisha vurugu na kuongoza wananchi kupiga mtu hadi kufa, kwani kwa kufanya hivyo kunasabisha  kutoweka kwa usalama.
Aliwataka pia kuondokana na dhana ya kumwona polisi na kumwogopa bali ashirikiane nae kutatua nini matatizo ya uhalifu katika Tarafa zao pamoja na kushirikisha jamii ili kupata ukweli wa jambo Fulani.

Aidha Kamanda wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Wilaya ya Rorya, kebero Kassimu aliwataka viongozi  hao kusaidia katika mapambano dhidi ya Rushwa na si wao kuwa kichocheo cha kupokea Rushwa.


Katika kikao hicho yaliwekwa maazimio yao ikiwa pamoja na kuweka sheria ndogo ndogo, kutoa taarifa ya mapato na matumizi, Baraza la ardhi la kata litoe taarifa ya maendeleo  kila baada ya miezi mitatu  kwenye Baraza la maendeleo la kata, kutenga eneo la misitu, kuibua vyanzo vya mapato, kutenga hekali za mazao ya chakula kwa kila kaya na kuhamasisha wakazi ujenzi wa vyoo bora.


Friday, May 11, 2012


VIONGOZI  wa Halmashauri za Mkoa wa Mara wamepeana mbinu  na changamoto za kukabiliana na wimbi la kutowasili  katika vituo vyao vya kazi ,watumishi wa  halmashauri na  jinsi ya kuwasidia  katika vitu vyao vya kazi wanapotakiwa kazini.


Katika kongamono hilo la siku lililofanyika Mkoani hapa viongozi hao wameazimia kuweka jitihada za kuweka vivutio kwa ajili ya kuwapata na kuwabakiza(retention) watumishi  wapya na waliopo na kuboresha  utendaji kazi mahala pa kazi .


Akisoma hotuba kabla ya ufunguzi  wa kongamano hilo,Afisa rasilimali watu wa Taasisi ya Benjamini William Mkapa HIV/AIDS,issuja kilian alisema kuwa Taasisi imeona ni vyema Halmashauri zikajadili mafanikio na changamoto ili kuweka mikakati ya uboreshaji na kubadilishana mbinu mbalimbali.


Alisema kuwa Taasisi imepanga kujenga nyumba 10 za watumishi na kuajiri watumishi wa afya katika Wilaya za serengeti, Tarime na Bunda katika mwaka 2013/2014.


Akifungua kongamano hilo, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa, Buhanda Kichinda alisema kuwa Rasilimali watu ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa mipango ya kazi ambayo inalengakuboresha huduma mbalimbalui za jamii ikiwemo huduma muhimu ya afya kwa watanzania wote.

Aliongeza kuwa kuna upungufu mkubwa wa rasilimali watu na kwamba kunahitaji jitihada za mikakati ya madhubuti kwa ngazi zote ili kuhakikisha wanapatikana watumishi wanaokidhi mahitaji na wenye ari ya utendaji kazi.


Alisema kuwa kongamano hilo limeandaliwa katika wakati muafaka kwani halmashauri zinajitayarisha kutekeleza mpango kabambe itakayopitishwa ya mwaka 2012/2013 pia kupokea watumishi wapya kazini.
Aidha Halmashauri ziliwasilisha taarifa pamoja na mikakati inayohusu menejimenti ya rasilimali watu katika Halmashuri kwa kushirikiana na ofisi ya Raisi Menejimenti ya utumishi wa Umma na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuhakikisha inapata idadi inayokidhi ya rasilimali watu katika sekta ya Afya.


Taasisi ya Benjamini William Mkapa HIV/AIDS kwa kushirikina na Shirika la kimataifa la intra Healh Intenational, inatekeleza shughuli mbalimbali katika halmashuri za Wilaya, zikiwemo kutoa mafunzo ya menejiment ya Rasilimali watu,maadili katika sekta ya afya kwa timu za uendeshaji za shughuli za sekta ya afya, uhasiashaji wa ajira katika sekta ya afya na ajira za mikataba kwa watumishi na waalimu wa afya.


Wilaya ya Serengeti imejiwekea mkakati wa kujenga nyumba tatu za watumishi na kutoa motisha kwa wafanyakazi bora waliokaa kazini kwa mika 25 mfululizo na utumishi uliotukuka huku Wilaya zingine kama Rorya ikilalmikia madiwani kutotumia utaratibu wa kupima mtumishi( Opras) na watumishi kubadilishiwa vituo kabla ya kuwasili katika kituo chake kipya, huku Wilaya ya Tarime ikilamikia ucheleweshwaji wa majibu ya watumishi walioomba kazi baada ya kustaafu kutoka Wizarani wa Afya.