RORYA.
MADIWANI wa Halmashauri ya
Wilaya ya Rorya Mkoani Mara wamemtuhumu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya
Rorya, Daniel Chacha kutumia fedha vibaya zinazotolewa na Halmashauri kwenda
katika vituo vinavyotoa huduma ya afya kwa ajili ya kununua vifaa,dawa na
mahitaji mengine huku akidaiwa kutofikisha baadhi ya vifaa kwenye vituo.
Hayo yalibainishwa katika
kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika jana ambapo Madiwani walisema kuwa
kuna baadhi ya wakuu wa idara wamekuwa wakitumia vibaya fedha za Serikali
ambapo walisema kuwa kuna fedha ambazo zilitolewa kwa ajili ya miradi ya
maendeleo lakini hazitumiki ipasavyo.
Diwani wa kata ya Kyango’mbe
Emanuel Manyama,(Matongwe) CCM alisema kuwa kuna kiasi cha fedha Milioni 20
zilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Bitiryo lakini fedha
zilizoingizwa kwenye akaunti si kiwango
kamili kilichotolewa na Halmashauri.
“Kuna ndume tatu ambazo ni
tatizo kwenye Halmashauri DMO,DT na Mhandisi wa maji hawa watu ni wala fedha
kijiji cha Bitiryo zilitengwa Milioni
20 kwa ajili ya ujenzi cha kushangaza
fedha zilizoingizwa kwenye akaunti ya kijiji ni Milioni 17 tu Milioni 3
hazionekani zimebaki Halmashauri lakini
hapa kwenye kablasha naambiwa milioni 20 ziliingizwa kwenye akaunti ya kijiji
na zimetumika kujenga zahanati na wakati ni Milioni 17 zilizowekwa kwenye
akaunti naomba nielezwe hizo pesa zingine zimekwenda wapi na kwanini
hazikuwekwa kwenye akaunti”alisema Manyama.
Diwani wa viti maalumu Tarafa
ya Nyancha Pendo Odero CCM aliongeza kwa
kusema kuwa Mganga mkuu Chacha anatuhumiwa kwa kutofikisha fedha za vifaa na
dawa kwenye baadhi ya vituo vya afya nakwamba baada ya kufahamu tuhuma hizo alianza
kuwahamasisha wanafunzi kumfichia siri ya kutofika kwa fedha za vifaa.
“DMO kala pesa za Halmashauri
za kununua vifaa na hata dawa zilizotolewa kusambazwa vituoni hazijafika baada
ya yeye kugundua mambo yameharibika alichukuwa gari kwenda kuwahamasisha
watumishi na kuwadanganya waseme pesa na vifaa vimefika lakini mipango yake
ikavunjika akiwa safarini taarifa zikafika kwa mkurugenzi na Mwenyekiti wa
Halimashauri wakazyuia gari na kumtaka astishe zoezi hilo”alisema Odero.
Diwani wa kata ya Mirare
Peter Ayoyi( CCM),alilalamikia Madiwani kutopatiwa vitambulisho vya Bima ya
afya licha ya kuwa tayali walishatoa
fedha za malipo ya vitambulisho.
“DMO atueleze hatima ya
vitambulisho vyetu vya bima ya afya Madiwani tumeshalipa pesa 3,000 kwa kila
Diwani ambapo 3,000 zingine kwa kila Diwani,
Halmashauri inachangia jumla kila Diwani ni 6,000 tumetoa lakini
hatujaletewa vitambulisho na hivi karibuni nimeenda Bima ya afya Mwanza
wakasema hawajapokea fedha za Madiwani kutoka Rorya DMO tuambie pesa zetu
umezipeleka wapi.”alisema Ayoyi.
Hata hivyo Mganga Mkuu Daniel
Chacha alikwepa kujibu baadhi ya maswali huku maswali mengine aliyojibu kudaiwa
kutowaridhisha Madiwani ambapo kwa upande wa vitambulisho vya Bima ya afya alisema kuwa vitambulisho vimekataliwa kwa
madai kuwa hakuna mchango wowote uliowasilishwa
kwa ajili ya kupatiwa huduma hiyo ya vitambulisho.
Madiwani hao hawakuishia kwa
Mganga Mkuu pia walimvaa Mweka Hazina wa Halmashauri,Caiser Ninalwo na kumtuhumu kushindwa kusimamia fedha
zikiwamo asilimia 20 inayotolewa na Halmashauri kwenda katika vijiji ambapo
walimlalamika kuwa kumekuwa na upungufu wa fedha zinazotolewa kwenda kwenye
vijiji huku vijiji vingine vikidaiwa kutofikiwa na fedha .
“Miongoni mwa Madiwani
waliolalamika kutolewa kwa fedha kidogo
kwenye vijiji ni Diwani wa kata ya Ikoma Laurent Adriano (CCM) Diwani wa kata
ya Koryo Peter Sarungi (CCM) Diwani kata ya Kitembe Thomas Patrick( Chadema) Diwani
wa kata ya Kigunga Magesa Magige (CCM).
“Kuna fedha inayotolewa na
Halmashauri asilimia 20 kwenda kwenye vijiji lakini kila kwaka fedha zinapungua
vijiji 80 vinatakiwa kupa asilimia hiyo mwaka juzi zilitolewa Sh. 613000,mwaka jana zikatolewa tena Sh.430,000, ambapo mwaka huu zimetolewa Sh. 100,000, kiasi hicho ni kidogo hasa ukizingatia serikali imetupatia ruzuku ya
zaidi ya Milioni 300 na kuna vijiji vina
akaunti havikuingiziwa fedha na kuna
vijiji havina akaunti fedha zinakwenda wapi?alihoji Sarungi.
Madiwani hao waliomba
kupatiwa Nyaraka za fedha zinazotolewa ili kujua na kuthibitisha kiasi cha fedha zinazokwenda kwenye vijiji
kila mwaka mbapo hata hivyo Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Rorya
Andreas Madundo alikubali ombi lao na kukubali kutoa nyaraka za fedha
zinazotolewa kwa manufaa ya vijiji.
Wakati huo huo madiwani hao
wa halmashauri wamemlalamika Mhandishi wa Maji Emmanuel Masanja kwa kutokamika
kwa visam vya majia ambpo walisema kuwa kuna fedha zilizotumika katika uchimbaji
wa visima lakini hadi sasa visima hivyo havitoi maji.
Naye Diwani wa kata ya
kisumwa, Amwolo Malaki (NCCR) alisema kuwa jumla ya Sh. Milioni 80
zilitolewa kufufua mradi wa maji katika kijiji cha Malasibora na Nyanchabakenye
na kwamba fedha za ujenzi huo zimepotea bila kuwa na manufaa.
“Visima havitoi maji na
mashine ni mbovu haifanyi kazi na mkandarasi alipewa Milioni 40 lakini hakuna
kisima ambapo kimeishakamilika na ikatangazwa zabuni kwa mkandarasi mwingine na
yeye akapewa Milioni 40 akanunua mashine
ambayo nayo haikufanya kazi, fedha zimekwisha na hatujui fedha zingine tutapata
wapi, wananchi wanaendelea kupata kero ya maji” Alisema Malaki.
Aliongeza “Zaidi ya mika mitatu
an nusu maji hayapatikani kamati zmeudwa kufatia lakini hatua zozote
zilizochukuliwa madiwani wenzangu kwa machafu haya na kwa kuzingatia kanuni
naomba mniunge mkono baraza lijeuke kuwa kamati tuwajadili hawa watu DMO, DT,
na Mhandishi wa Maji tumechoka na utendaji wao mbovu kwani kila baraza
tunazungumzia mambo yale yale yasiyotekelezwa?Alisema.
Hata hivyo kutokana na majibu
yaliyotolewa na wakuu hao wa Idara hizo tatu hayakuweza kuwaridhisha madiwani
hali iliyolazimu baraza hilo
kugeuka na kukwa kamati ili kuwajadili kwa kina.
No comments:
Post a Comment