HALMASHAURI ya Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara, imetakiwa
kuongeza vyanzo vyake vya mapato ili iweze kujitosheleza yenyewe katika sehemu
kubwa ya matumizi si ya kutegemea ruzuku toka serikalini.
Akiwasilisha taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali (CAG) kuhusu taarifa ya fedha za halmashauri ya Wilaya ya Tarime
kwa mwaka wa fedha uliouishia Juni 30 2011 Mkaguzi Mkazi Msaidizi Mkoa wa Mara,
Deogratius Waijaha alisema kuwa asilimia 91.4 ya halmshauri inategemea ruzuku
kuu, hivyo lazima ianzishe na kubuni mipango ya kuifanya ijitegemee na sio
kutegemea ruzuku kutoka Serikali kuu.
Waijaha alisema kuwa mapato ya ndani ambayo ni Sh. Bilioni
1,503,489,981 ni madogo sana
ukilinganisha na ruzuku inayopewa halmashauri kutoka Serikali kuu ya kiasi cha
Sh. Bilioni 20, 960, 601,198.
Kwa upande wa matumizi ya kawaida alisema kuwa halmashauri
ilitumia kiasi ch Sh. 17,604,608,018 kwa matumizi ya kawaida wakati ambapo mapato
yake ya kawaida yalikuwa Sh. Bilioni
18,238,072,617 ikionyesha kwamba kulikuwa na Balance ya Sh. 633,
464,599.
Mkaguzi huyo alisema kuwa kwa mwaka wa fedha 2010/2011
halmashauri ilikusanya Jumla ya Sh. 1,503,489,981 kutoka katika vyanzo vyake
ukilinganisha na bajeti yake ya Sh. 1,263,405,000 na kusababisha makusanyo
zaidi ya Sh. 240,084,981 yakiwa sawa na asilimia 19.
Maeneo ya faini na tozo yalibajetiwa kukusanya kiasi cha Sh.
583,405,00 lakini kiasi kilichokusanya
kilikuwa Sh. 549,769, 083 ikiwa na upungufu wa Sh. 33,635, 916 sawa na 5.8 ambapo kodi ya ndani
ilibajetiwa kiasi cha Sh. 680,000,000 lakini kiasi kilichokusanywa kilikuwa na
Sh. 868,036,449 ikiwa ni ongezeko zaidi
ya Sh. 188, 036,449 ikiwa ni sawa na asilimia 27.7
Mkaguzi Waijaha alisema kuwa halmashauri imepata hati
inayoridhisha ambapo aliipongeza kwa kusimamia vyema rasilimali na fedha za
halmashauri na kwamba hali ya fedha ya halmashauri hadi Juni 30 2011 na kwamba
matokeo ya utendaji na mapato halisi kwa mwaka ulioishia inawiana na viwango
vya kimataifa vya uandaaji wa hesabu za fedha kwa sekta ya Umma.
Pia alisema katika manunuzi yenye jumla ya Sh. 32,050,000
yaliyokusanywa kupitia programu ya maendeleo ya kilimo (ASDP) yalikiuka kanuni Na.
49 ya manunuzi ya umma ya mwaka 2005 kwa kununua vifaa huska katika kiasi
kidogo kidogo kupitia hati mbalimbali za malipo badala ya kufuata taratibu za
Zabuni kama ilivyokuwa ikihitajika na
kanuni husika.
No comments:
Post a Comment