Watangaza nia ya Uenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya wameaanza
kutumia mbinu za kuhujumiana wao kwa wao huku wakitumia baadhi ya vyombo vya
habari kuchafuana.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hii ofisini kwake, Katibu
Mwenezi wa CCM Wilaya ya Rorya Samueli kiboye alisema kuwa mmoja ya mgombea
ambaye hakutaka kutaja kutaja jina lake
alisema ameanza kutumia
vibaya vyombo vy ahabari kwa kukiuka taalumu hiyo.
Alisema kuwa kuna moja ya gazeti la kila siku si Uhuru,limetoa habari kuwa amemkatisha masomo
mwanafunzi na kumfanyisha kazi za nyumbani, huku binti huyo akinusha habari
hizo kuwa yeye aliamua kuondoka nyumbani kwao kutokana vipigo vya mara kwa mara
kutoka kwa Baba Mzazi kumkatisha masomo na
kumlazimsha kuolewa na ndipo
binti huyo alipoamua kutafuta kazi za nyumbani.
“Baada ya Mama yangu mzazi, Wankuru Joseph kufarikia Mwaka
2008,nilibahatika kuchaguliwa na kujiunga na Shule ya Sekondari Nyandoto-Tarime
kidato cha kwanza mwaka 2009, hadi cha Tatu sikuwahi kulipiwa ada na mzazi, walimu
wakamwandikia barua ya kumtaka alipe ada na wito wa kumwita shuleni lakini
hakufanya hivyo, nikafukuzwa shuleni na akaniambia kuolewa nilipokataa
alinipiga sana na Kunifukuza alisema Angelina.
Aliongeza kuwa baada ya kufukuzwa na baba yake alitafuta
sehemu ya kuishi na kumpata msamalia mwenye ambaye ni Mke wa Katibu Mwenezi wa
CCM Wilaya na kumwambia matatizo yake na kuamua kuishi hapa hadi sasa.
Alisema kuwa hiyo ni hujuma kutoka na watangaza nia wenzake kudurufu
( Photocopy) kwa habari iliyotolewa na kuisambaza katika vijiji ili wananchi waisome
kwa nia kum dhoofisha kisiasa.
Aidha amewataka waandishi wa habari kutumia taaluma yao ya kuandika habari
sahihi na kwamba wasitumike kwa lengo la masilahi ya mtu binafsi.
Fomu za kugombea
nafasi mbalimbali za uongozi kwa ngazi ya Wilaya na Mkoa zitaanza kuchukuliwa Juni
2 Mwaka huu, ambapo mpaka sasa miongoni mwa wagombea wa kiti cha Uenyekiti
Wilaya ya Rorya ni Samuel kiboye (Namba
tatu), Razaro Akuku, Jamoko Kateti na Yoda Ambonya.
No comments:
Post a Comment