VIONGOZI wa
Halmashauri za Mkoa wa Mara wamepeana mbinu na changamoto za kukabiliana na wimbi la kutowasili
katika vituo vyao vya kazi ,watumishi wa halmashauri na jinsi ya kuwasidia katika vitu vyao vya kazi wanapotakiwa kazini.
Katika kongamono hilo la siku lililofanyika Mkoani hapa
viongozi hao wameazimia kuweka jitihada za kuweka vivutio kwa ajili ya kuwapata
na kuwabakiza(retention) watumishi wapya
na waliopo na kuboresha utendaji kazi
mahala pa kazi .
Akisoma hotuba kabla ya ufunguzi wa kongamano hilo,Afisa rasilimali watu wa Taasisi
ya Benjamini William Mkapa HIV/AIDS,issuja kilian alisema kuwa Taasisi imeona
ni vyema Halmashauri zikajadili mafanikio na changamoto ili kuweka mikakati ya
uboreshaji na kubadilishana mbinu mbalimbali.
Alisema kuwa Taasisi imepanga kujenga nyumba 10 za watumishi
na kuajiri watumishi wa afya katika Wilaya za serengeti, Tarime na Bunda katika
mwaka 2013/2014.
Akifungua kongamano hilo, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa,
Buhanda Kichinda alisema kuwa Rasilimali watu ni nguzo muhimu katika
utekelezaji wa mipango ya kazi ambayo inalengakuboresha huduma mbalimbalui za
jamii ikiwemo huduma muhimu ya afya kwa watanzania wote.
Aliongeza kuwa kuna upungufu mkubwa wa rasilimali watu na
kwamba kunahitaji jitihada za mikakati ya madhubuti kwa ngazi zote ili
kuhakikisha wanapatikana watumishi wanaokidhi mahitaji na wenye ari ya utendaji
kazi.
Alisema kuwa kongamano hilo limeandaliwa katika wakati
muafaka kwani halmashauri zinajitayarisha kutekeleza mpango kabambe itakayopitishwa
ya mwaka 2012/2013 pia kupokea watumishi wapya kazini.
Aidha Halmashauri ziliwasilisha taarifa pamoja na mikakati
inayohusu menejimenti ya rasilimali watu katika Halmashuri kwa kushirikiana na
ofisi ya Raisi Menejimenti ya utumishi wa Umma na Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii kuhakikisha inapata idadi inayokidhi ya rasilimali watu katika sekta ya
Afya.
Taasisi ya Benjamini William Mkapa HIV/AIDS kwa kushirikina
na Shirika la kimataifa la intra Healh Intenational, inatekeleza shughuli
mbalimbali katika halmashuri za Wilaya, zikiwemo kutoa mafunzo ya menejiment ya
Rasilimali watu,maadili katika sekta ya afya kwa timu za uendeshaji za shughuli
za sekta ya afya, uhasiashaji wa ajira katika sekta ya afya na ajira za
mikataba kwa watumishi na waalimu wa afya.
Wilaya ya Serengeti imejiwekea mkakati wa kujenga nyumba
tatu za watumishi na kutoa motisha kwa wafanyakazi bora waliokaa kazini kwa
mika 25 mfululizo na utumishi uliotukuka huku Wilaya zingine kama Rorya
ikilalmikia madiwani kutotumia utaratibu wa kupima mtumishi( Opras) na
watumishi kubadilishiwa vituo kabla ya kuwasili katika kituo chake kipya, huku
Wilaya ya Tarime ikilamikia ucheleweshwaji wa majibu ya watumishi walioomba
kazi baada ya kustaafu kutoka Wizarani wa Afya.
No comments:
Post a Comment