VIONGOZI wa Tarafa,Kata vijijiji na Vitongoji wa Wilaya ya
Rorya wamepata Mafunzo juu ya Utawala Bora na uwajibika , ulinzi shirikishi na
rushwa katika eneo lao la kazi.
Akitoa mafunzo hayo ya siku mbili yaliyofanyika katika
kijiji cha Sudi Tarafa ya Mirare Wilayani humo, Afisa Utumishi wa Wilaya hiyo,
Sebastian Masanja aliwataka viongozi hao
kuwatumikia wananchi wao na kuhakikisha wanatoa taarifa za mapato na matumizi
kwa wananchi kwenye mikutano mikuu ya vijiji WDC na taarifa zote na michango ya
wananchi,tozo, wahisani,Halmashauri na Serikali kuu.
Alisema kuwa upo udhaifu wa kutofanya vikao ambao unasababisha
kuwepo kwa ugomvi hasa wa ardhi na kutokusanya ushuru kwa maduka na migahawa
iliyopo katika vijiji hivyo.
Aliwataka viongozi hao kuweka utaratibu wa kuwajibishana
kati ya viongozi wa kuchaguliwa na wananchi pamoja na watumishi wa Umma.
Aidha aliwataka viongozi hao kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwa
na mashamba ya mfano, miradi midogo midogo ya kuwawezesha kujikimu katika
familia zao kama ufugaji wa kuku, bata na mbuzi ili wananchi waige mfano wao,
kwani kwa kufnaya hivyo itawasababisha kuondokana na umasikini.
Pia amewahimiza kuachana na mila potofu ya kuridhi wajane
kwani kwa kufanya hivyo ni kuongeza ongezeko la waathirika wengi wa Ugonjwa wa
Ukimwi ukizingatia kuwa Wilaya ya Rorya ndiyo yenye maambukizi makubwa
kiwilaya.
Aidha aliwataka kusaidia kampeni mbalimbali za kitaifa mfao,
kupima VVU, chanjo za watoto, panga uzazi, kuwa na choo bora, kuchemsha maji ya
kunywa, kunawa mikono kwa sabuni, kuwa waaminifu katika mapenzi na kuacha
vitenndo vya uzinzi, kujitolea kwenye shughuli za maendeleo, kuvaa mavazi yenye
heshima, kuazisha vikundi yva ulinzi shirikishi jamii na kupiga vita rushwa.
Akitoa mada juu ya ulinzi shirikishi,Mkaguzi Msaidizi wa
jeshi la polisi, Antony kahema aliwataka viongozi hao kuacha tabia ya
kujichukuliwa mamlaka na kuwanyanyasa wananchi kwa mamlaka waliyopewa na badala
yake wawafikishe katika mikono ya sheria.
“Nashangaa wapo baadhi ya watendaji wa kata na vitongoji na
vijiji wamekuwa wakiwanyanyasa wanachi aidha kwa kuwapiga na kuwafungia masaa
24 katika ofisi zao wale wanaosaidikiwa kuwa na tuhuma, hili ni kosa kwani kazi
yenu ni kuwasiliana na jeshi letu ili hatua za kisheria zichukuliwe na si
kuwapiga hadi kusababisha maumivu makali.”Alisema Mahema.
Aliwataka kuwa na utii wa sheria pasipo kuwa na shuruti na
si kiongozi kuhamasisha vurugu na kuongoza wananchi kupiga mtu hadi kufa, kwani
kwa kufanya hivyo kunasabisha kutoweka
kwa usalama.
Aliwataka pia kuondokana na dhana ya kumwona polisi na
kumwogopa bali ashirikiane nae kutatua nini matatizo ya uhalifu katika Tarafa
zao pamoja na kushirikisha jamii ili kupata ukweli wa jambo Fulani.
Aidha Kamanda wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),
Wilaya ya Rorya, kebero Kassimu aliwataka viongozi hao kusaidia katika mapambano dhidi ya Rushwa
na si wao kuwa kichocheo cha kupokea Rushwa.
Katika kikao hicho yaliwekwa maazimio yao ikiwa pamoja na
kuweka sheria ndogo ndogo, kutoa taarifa ya mapato na matumizi, Baraza la ardhi
la kata litoe taarifa ya maendeleo kila
baada ya miezi mitatu kwenye Baraza la
maendeleo la kata, kutenga eneo la misitu, kuibua vyanzo vya mapato, kutenga
hekali za mazao ya chakula kwa kila kaya na kuhamasisha wakazi ujenzi wa vyoo
bora.
No comments:
Post a Comment