WAKUU wapya wa Wilaya Mkoa wa Mara jana waliapishwa rasmi na
Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa tayari kwa kuanza kazi, iliyofanyika katika
Ukumbi wa Uwekezaji wa Mkoa wa Mara, uliopo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Baada ya kuapishwa
kwa Wakuu hao wapya wa Wilaya kwa pamoja walikwenda katika ofisi za CCM Mkoa
kuweka saini katika kitabu cha wageni jambo ambalo ni mara ya kwanza kufanya hivyo,tofauti
na awali kwa kwenda kila mmoja kwa muda wake na siku tofauti.
Shamra Shamra za
kuwaapisha Wakuu hao wapya zilitia fola, kwa wananchi na viongozi mbalimbali waliofurika
katika ukumbi huo, jambo ambalo pia liliwashangaza baadhi ya viongozi na kwamba
halijawahi kutokea.
Sherehe hizo zilianza kwa dua kutoka katika viongozi wa
madhehebu ya dini ya kiislamu na kikrsito ambapo Shehe Mkuu wa Waisalamu Mkoa
Shehe Magehe aliomba dua, akifuatiwa na Askofu Mkuu wa Wakatoliki, Mhashamu Msonganzila.
Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka Wakuu hao wa Wilaya
kuwajibika kwa kufanya kazi kwa
uadilifu, uchapa kazi, kuwa na moyo wa kujituma, maono na kuacha alama kama
kumbukumbu zao waachapo madaraka na kuwahudumia wananchi ipasavyo kwani Rais Jakaya Kikwete amewaamini
wao.
Alisema kuwa kuna changamoto zinaukabilia Mkoa wa Mara hasa
kwa ulinzi na usalama japokuwa bado kuna matukio yanayofanyika lakini yanadhibitiwa
haraka.
Alisema kuwa kuna baadhi ya watu kutoka mikoa na Wilaya
zinazopakana na nchi jirani wanaingia katika Mkoa wakiwa na silaha na risasi
ambapo jumla ya risasi zipatazo 430 na SMG tatu zilikamatwa katika Wilaya za
Tarime na Serengeti na kubaini watuhumiwa hao ni wakazi wa Kigoma.
Alizitaja changamoto zingine zinazoukabili Mkoa wa Mara,
pamoja na kuwa na rasilimali za kutosha wananchi wake bado ni masikini ambapo
Mkoa huku chini ya kiwango cha kitaifa, kuvushwa kwa magendo katika Wilaya ya Tarime kwenda
nchi jirani ya Kenya na ajira kwa vijana.
“ Kuhusu ajira wapo vijana ambao hawataki kujishughulisha na huwa vijiwe asubuhi , hii ni changamoto kubwa, huku
kukiwa na fursa nyingi za Mkoa kwa wao kujishughulisha, kuwepo wazi kwa maeneo
ya kilimo, huku ardhi ikiwa na rutuba ya kutosha” Alisema Tuppa.
Aliwataka Wakuu hao wapya kushughulikia changamoto hizo kwa
pamoja kwa kushirikiana na wadua mbalimbali wa maendeleo wa Mkoa wa Mara.
Walioapishwa majina yao na sehemu zao za kazi zikiwa kwenye
mabano ni ni Joshua Chacha Mirumbe(Bunda), Angelina Mabula (Butiama), Jackson Msome(
Musoma), Alias Goroe( Rorya), Capt. Mstaafu James Yamungu (Serengeti) na John
Henjewele( Tarime).
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa walihudhuria sherehe
hizo wakiwemo pia viongozi wa vyama vingine vya siasa.
No comments:
Post a Comment