MUSOMA
WANANCHI wa Mkoa wa
Mara, wametakiwa kufahamu utaratibu wa kisheria wa wafugwa wenye kifungo kirefu
wanaoonyesha mwenendo mzuri wa kurekebika wawapo Magereza (PAROLE), na kumaliza
kifungo chao wakiwa nje ya gereza na si kuwakataa.
Hayo yalisemwa Mei 29 Mwaka huu katika uzinduzi wa Bodi ya Parole, Afisa
Mwandamizi Afisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Buhacha Kichinda alipokuwa anazindua
bodi hiyo yenye jukumu la kupitia majalada ya wafugwa wenye nidhamu wawapo
katika vifungo vyao magerezani.
Alisema hiyo ni changamoto kubwa inayowakabili wafugwa
wanaoachiwa kwa sheria ya Parole kukataliwa na wananchi wanapotakiwa kumalizia
kifungo chao wakiwa majumbani mwao, jambo ambalo lilikuwa kikwazo kwa utekelezaji
wa sheria hiyo.
Aliongeza kuwa elimu inahitaji kwa wananchi juu ya umuhimu
wa Parole kwa kushirikiana na viongozi wa Serikali ili wananchi waweze
kushirikiana nao kwani wamekuwa tayari wamehakikiwa kuwa wana tabia hivyo na
wengi kujishughulisha katika majukumu
mbalimbali ya ujenzi wa Taifa kwa kujishughulisha na kilimo, ufugaji, uvuvi
na biashara ndogo ndogo.
Ameitaka bodi hiyo kufanya kazi za uchunguzi wa majalada kwa
kina ili wafugwa hao wanapokuwa na kifungo cha nje wasifanye uhalifu tena na
kusababisha kutoaminiwa kwa bodi.
Awali akisoma taarifa ya Parole, Mkuu wa Magereza Mkoa (RPO), Melchadus Mwendwa alisema kuwa
ofisi yake imekuwa na changamoto mbalimbali za kufuatilia taarifa muhimu za
kukamilisha majalada ya wafugwa wanaopekezwa kuachiliwa ikiwa ni pamoja na
upatikanaji wa nakala za hukumu toka Mahakamani,taarifa za uhalifu za awali
toka jeshi la polisi,ufinyu wa bajeti na uelewa mdogo wa Sheria ya Parole kwa
viongozi wa vijiji/mitaa anapochagua kuishi mfugwa.
Alisema kuwa kati ya wafugwa 268 wafugwa 10 tu waliovunja masharti wengi wao
wakitenda makosa mengine ya jinai na kuwalazimu kurudishwa gerezani kwa mujibu
wa sheria na wafugwa wapatao 40
wakiendelea na vifungo vyao chini ya utaratibu wa Parole wakiwa katika mitaa na
vijiji walipochagua kuishi na wafugwa
wapatao 219 tayari wamemaliza vifungo vyao chini ya utaratibu huo.
Sheria ya Bodi ya Parole N0. 25/1994 na marekebisho yake No.
5/2002, kanuni za bodi ya Parole No. GN 563/1997 vilianza kutumika mwaka 1999
na kwa mujibu wa kifungu cha 3(3) cha Sheria ya Bodi za Parole kinaidhinisha
ziundwe Bodi za Parole Mikoa ambayo kwa Mkoa wa Mara zilizinduliwa Mei 29
ambayo kazi zake ni kupitia kila jalada
la mfugwa lenye vielelezo vinavyojitajika toka sehemu mbalimbali,
aliyependekezwa kuachiliwa kwa Parole na kuthibitisha viwango vya sifa za
mfugwa ili akubalike.
Aidha kati ya majalada ya wafugwa wapatao 321 yaliyopekezwa
na Bodi ya Parole Mkoa wa Mara tangu utaratibu huo uanzishwe ni majalada 22 tu
ambayo bado yapo kwenye Bodi ya Parole Taifa yanayofanyiwa mchakato wa
kuyapeleka kwa Waziri huska ili ayatolee uamuzi idadi ambayo hairidhishi.
No comments:
Post a Comment