Thursday, May 31, 2012

SAKATA LA KUMKATAA DC TARIME LAGONGA MWAMBA

SAKATA LA KUMKATAA  DC TARIME LAGONGA MWAMBA
TARIME.

SAKATA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Tarime Mkoani Mara la
kumkataa na kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete kumwondoa Ukuu wa Wilaya,
Mkuu wa Wilaya John Henjewele limeingia sura mpya baada ya madiwani
kugawanyika wengine wakitaka aondolewe na huku wengine wakiomba  apewe
muda wa kujibu tuhuma zinazomkabili.



Licha ya kuwa kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichopita Mei 08
2012 madiwani wa CCM pamoja na wa kambi ya upinzani waliungana pamoja
kujenga hoja ya kutaka Henjewele kuondolewaTarime,kwenye kikao
kilichofanyika Mei 30 ambapo baada ya  hoja hiyo kugusiwa na madiwani
toka kambi ya upinzani iliwagawa madiwani ambapo madiwani toka CCM
waliwageuka wale wa Chadema.



Kwa hali hiyo Madiwani wakambi ya upinzani walijikuta wanaingia wakati
mugumu walipojaribu kukumbushia msimamo wao wa maazimio ya kikao
kilichopita ambapo madiwani wote kwa pamoja walikuwa na kauli moja ya
kumkataa Henjewele,CHADEMA walijikuta CCM wanawageuka kwa madai kuwa
hoja hiyo haikuja  kwa wakati mwafaka.



Kufuatia utata huo ambao ulisababisha kikao kuonyesha hali ya
kutokalika na  malumbano ya kwa baadhi ya  madiwani hasa wa kambi ya
upinzani huku wakitishia kususia kikao na kujigeuza kuwa kamati hali
ambayo ilimlazimu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Fidelis Lumato
kusoma kanuni namba 17 yenye kumpat fursa Mwenyekiti kumwondoa Diwani
yeyote  anaye leta fujo ndani ya kikao kwa  kumtaja kwa jina ili
achukuliwe hatua ikiwa ni pamoja na kutolewa nje ya kikao na
kutohudhuria vikao vitatu mfululizo katika baraza hilo, hali iliyo
leta utulivu nakuendelea na kikao.



Sagara alilazimika kuwa mkali baada ya kanuni kusomwa kuwa anaye kiuka
utaratibu na kuvuruga kikao lazima awajibishwe kwa mjibu wa kanuni
ambapo sagara alitishia madiwani mawili toka kambi ya upinzani kutoka
nje ya kikao kwa kuwa wanaonekana kuvuruga kikao baada ya hapo Diwani
Mang'enyi Ryoba  toka kata ya Nyanungu(Chadema)  kuwatetea wenzake
kuwa awasamehe ilikuendelea na kikao na kwamba ni changamoto kwao,
ambapo Mwenyekiti aliridhia ombi hilo na kuwasamehe ili kuendelea na
kikao.



Aidha kwa kuhitimisha mjadala huo ulioleta utata huku baadhi ya
madiwani toka kambi ya upinzani wakisimama bila ruksa ya Mwenyekiti
midhili ya nyumbu, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Amosi Sagara
aliwataka Madiwani kufuata utaratibu kwa kuunda kamati itakayo kwenda
kwa  Mkuu wa Mkoa John Tuppa ili wapate  majibu kuhusiana na maazimio
ya kikao kilicho pita .

Awali Madiwani hao waligomea kikao kilichopita kwa   kumtuhumu Mkuu wa
wilaya John Henjewele kuwa ameshindwa kuondoa kizuizi cha polisi
kilichopo kijiji cha  Magena kwa madai kuwa hakina msaada wowote na
wananchi.

kikao hicho kilihusu ripoti ya ukaguzi wa hesabu za Serikali na
kupitia miradi ya mwaka wa fedha ya mwaka 2010/2011.

No comments:

Post a Comment