TARIME.
KUFUATIA kuundwa kwa kikosi kazi (Task Force) kutoka Wizara
ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuchunguza uthamini fidia ya wakazi
wanaozunguka mgodi wa Dhahabu wa North Mara,wananchi hao sasa watapatiwa
ufumbuzi wa tatizo hilo.
Hayo yamesema na Afisa Mthamini Mkuu wa Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mwenyekiti wa Kikosi kazi hicho, Adam Yusuf
alipokuwa akijibu hoja ya Diwani wa kata ya Mbogi,Wilaya ya Tarime Mkoa wa
Mara Sylivester Nyankomo,katika kikao
cha Baraza la Madiwani, kuhusu fidia utatuzi wa mgogoro wa Mgodi na wananchi wanaozungumka
katika eneo hilo.
Katika hatua nyingine Diwani huyo pia alikishtumu Kikosi
kazi hicho kwa kutoa taarifa isiyo na sahihi wala uthibitisho kutoka kwa
mwekezaji,jambo ambalo lilizua mgogoro katika kikao hicho na madiwani kuitaka
taarifa hiyo iandikwe na kuwekewe sahihi ndipo ijadiliwe.
Akisoma taarifa hiyo mbele ya baraza la madiwani wa
halmashauri ya Wilaya ya Tarime,katika kikao cha dharula cha kupokea taarifa ya
vikao kati ya kikosi kazi cha
kushughulikia masuala ya uthamini na fidia, Katibu wa kikosi kazi,
Jeremiah Minja alisema kuwa ni lengo la
Serikali kuona kuwa matatizo yaliyojitokeza katika mgodi wa Noth Mara yanapatiwa
ufumbuzi wa kudumu na kumwezesha mwekezaji kuendelea na shughuli zake kama
kawaida huku haki stahili za wananachi wa ardhi wanaozunguka mgdo huo
zikizingatiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.
Aidha ni azam ya
Serikali ni kuona kuwa amani na Utulivu na mahusiano mema kati ya Mgodi
na wananchi wanaozunguka Mgodi huo vinadumishwa
na ndiyo maana ikaazimia kiudwe kikosi kazi kitakachojumisha wataalamu
na
maafisa kutoka katika taasisi mbalimbali za Serikali kusimamia utatuzi
wa
matatizo hayo.
Alisema kuwa matatizo yaliyojitokeza katika maeneo ya vijiji
vinavyozunguka mgodi ni pamoja na wanachi ambao maeneo yao yalifanyiwa uthamini
lakini bado hawako tayari kuchukua malipo yao,waliofanyiwa uthamini lakini
hawako tayari kuondoka,waliopokea sehemu ya malipo nab ado wako katika maeneo
yaliyofanyiwa uthamini,waliofanyiwa uthamini wakachukua malipo yao yote na
kuwaendelea kukaa na kuendeleza maeneo ambayo yalifanyiwa uthamini ambapo kuna
wengine hawako tayari kuona maeneo yao yakifanyiwa uthamini.
Wiki iliyopita katika kikao cha Baraza la Madiwani wakati wa kutambulisha kikosi kazi hicho,
Baraza liliagiza kikosi hicho kwenda katika vijiji vya Kewanja, Nyangoto na
Nyakunguru na Baraza lipewe matokeo ya vikao hivyo kabla ya zoezi rasmi la
uthamini na uhakika kuanza katika maeneo husika.
Alisema kuwa baada ya kikao cha halamshauri ya Kijiji cha
Kewanja kulitolewa hoja na kujdiliwaambapo iliagizwa Uthamini ufanyike ndani ya
wiki mbili,ambapo kikosi hicho kilifanya kazi hiyo kama kilivyoagizwa lakini
dosari iijitokeza katika kijiji cha Nyangoto ambao hawakuwa tayari kuzungumza
wala kushirikia katika zoezi hilo hadi
hapo Mgodi utakapotoa kesi yao Mahakamani na ndipo kipagwe kikao kingine na
uongozi wa mgodi uwepo ili kuzungumza nao.
Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Halmashauri
hiyo, Amos Sagara aliiomba Wizara ya Nishati na Madini ,Baraza la Mazingira
(NEMC), wao pia waunde kikosi kazi kingine kwa ajili ya kuchunguza matatizo
yanayowakabili wakazi wanaozunguka mgodi huo kwani maisha yao yako hatarini kwa
kuwa maji machafu ya kusafishia dhahabu
yanaathiri afya ya watanzania hao ambao hawana hatia.
Aidha alikiomba kikosi kazi hicho kuzunguka kwa vijiji vyote
vinavyozunguka Mgodi huo ili kujua matatizo yao ingawaje nayo yanafafa na ya vijiji
hivyo, vijiji ambavyo ‘Task Force’ imetakiwa kwenda na kurudisha mrejesho ni pamoja na Kerende, Nyamwaga,
Matongo, na Genkuru.
Akizungumza katika Kikao hicho, Meneja wa Mgodi huo,Champman
Gerry alitoa shukrani kwa Serikali kuunda timu hiyo ili kuja kutatua matatizo kwamba amesikia akilalamikiwa kuwa
walikuwa hawalipwi fidia kwa mujibu wa sheria,na kwamba atazingatia utaratibu
atakaopewa na kwamba ataufuata ili kuondoa kabisa matatizo yaliyopo baina
yao na wananchi.