Friday, November 23, 2012

WASIFU WA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM BARA.


WASIFU WA PHILIP JAPHET MANGULA (MAKAMU MWENYEKITI CCM BARA)

KUZALIWA:

NDUGU Philipo Japhet Mangula , alizaliwa Tarehe 31 Machi 1941 katika kijiji cha Imalimnyi, Wilaya ya Wanging'ombe, Mkoa wa Njombe.

ELIMU NA MAFUNZO MBALIMBALI:
Mwaka 1950-1953 Alisoma katika Shule ya Msingi Kidugala, Wilaya ya Wanging'ombe,Mkoa wa Njombe.

Mwaka 1754-1957 Alisoma Shule ya Kati 9Middle School) ya Bulogwa Wilayani Makete.Mwaka 1957 alihamia Shule ya Kati ya Mpwapwa alipomiazia elimu yake ya darasa la Nane.

Mwaka 1958-1959 Alisoma Shule ya Sekondari ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.

Mwaka 1960-1961 Alisomea Ualimu katika Chuo cha Ualimu Mpwapwa Mkoani Dodoma.

Mwaka 1966 April-Dec Alihuduria kozi ndefu ya masuala ya Siasa na Uongozi katika Chuo cha TANU, Kivukoni.
Mwaka 1967 Jan-Machi Alihudhuria mafunzo ya Kijeshi katika kambi y ajeshi la kujenga Taifa, Mgulani.Hiyo ilikuwa Operesheni Azimio.

Mwaka 1967 April-Juni, alirudi tena katika Chuo cha TANU Kivukoni kwa ajili ya Mafunzo Maalumu ya Ualimu wa Siasa. Baada ya mafunzo hayo aliteuliwa kuwa Mwalimu wa Siasa katika Mkoa wa Iringa.

Mwaka 1973-1976 Alisoma Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya na kuhitimu katika fani ya Mawasiliano ya Umma (Mass Communication).

KAZI NA MAJUKUMU MBALIMBALI

Mwaka 1962-1964 Alikuwa Mwalimu wa Shule ya kati (Middle School) ya Ntaba, Wilaya ya Rugwe, Mkoani Mbeya.

Mwaka 1965 Jan-Dec. Alikuwa Mwalimu wa Shule ya kati ya Mano, Wilaya ya Rugwe, Mkoani Mbeya.

Mwaka 1966 Jan-April Alikuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Gangilonga, Iliyoko Iringa Mjini.

Mwaka 1967 July-Dec Alikuwa Mwalimu wa Siasa katika Mkoa wa Iringa.

Mwaka 1968-1977 Alikuwa Mwalimu wa Siasa katika Chuo cha TANU, Kivukoni.Katika kipindi hicho alishika nyadhifa mbalimbali Chuoni hapo zikiwemo:-

  • Mkuu wa Idara ya Propaganda
  • Mwendeshaji kipindi cha Elimu ya Umma Radioni kilichojulikana kama FIMBO YA MNYONGE
  • Mhariri wa Majarida ya MBIONI,UJAMAA pamoja na Jarida Maalumu lililotolewa kwa lugha ya kiingereza ili kuhamasisha harakakati za Ukombozi Kusini mwa Afrika,lililokuwa likiitwa THE RATIONAL CHOICE.
  • Mwaka 1971,Aliteuliwa kwenda mstari wa mbele katika Jimbo la Cabo Delgado Msumbiji kushuhudia vita ya Ukombozi nchini humo.
Mwaka 1977-1983 Aliteuliwa kuwa Katibu wa CCM wa Wilaya na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Mkoani Mwanza.

Mwaka 1983-1986 Aliteuliwa kuwa Makamu wa Mkuu wa Chuo cha CCM Kivukoni na Mkuu wa Mafunzo Chuoni hapo.

Mwaka 1986-1991 Aliteuliwa kuwa Katibu wa CCM wa Mkoa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Mwaka 1992-1996 Aliteuliwa tena kuwa Katibu wa CCM wa Mkoa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Mwaka 1996-2006 Alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

Katika Kipindi choye hicho,Ndugu Mangula alisimamia kazi za Chama za Utendaji kwa umakini, umahiri, uhodari na uadilifu wa hali ya juu.

Ndugu Mangula akiwa ndiye mkurugenzi Mkuu wa uchaguzi ndani ya Chama, alisimamia kwa ustadi mkubwa kampeni za uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika amjimbo 31 nchini, ambapo kati ya majimbo hayo CCM ilipoteza majimbo mawili tu.
Aidha, Ndugu Mangula aliteuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Kitaifa ya Kampeni za CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu 2000 na akateuliwa tena kufanya kazi hiyo hiyo mwaka 2005.Katika Chaguzi hizo CCM ilishinda kwa kishindo.

Ndugu, Philipo Japhet Mangula amekuwa Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM kuanzia Mwaka 1984 alipochaguliwa kwa mara ya kwanza hadi 2007 ambapo aliamua kurudi kijiji kwake na kuwa Mkulima.

Wanachama wengine waige mifano hiyo si kujaza malaver 4 majumbani mwao huku wakiwadharau wakulima na wakati bila jasho la wakulima hawawezi kushika usukani kuendesah magari hayo.

HONGERA! MKULIMA WA MBOGA MBOGA NA MATUNDA TEKELEZA AHADI ZAKO ZA KUWASHUGULIKIA MAFISADI VINGINEVYO...............???????????

Wednesday, November 14, 2012

MUKAMA ATOLEWA UKATIBU MKUU CCM.

DODOMA.


Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM,Wilson Mukama ametolewa katika Uongozi huo na nafasi yake kuchukuliwa na Abdulahman Kinana.

Mukama ni Katibu Mkuu wa kwanza aliyewahi kukaa kwa muda mfupi,ambapo amedumu kwenye kiti kwa muda wa Mwaka Mmoja tu. 

Habari kutoka hapa Dodoma zimesema kuwa katibu Mkuu huyo ametolewa kutokan ana kutokuwa mahiri katika kujibu hoja za wapinzani.

Naibu katibu Mkuu Bara, amekuwa Mwigulu Nchemba, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, amekuwa Ally Vuai ,Huku Nape Nnauye amebaki na nafasi yake ya Uenezi,huku nafasi ya January Makamba ya Mahusiano ya Nje ikichukuliwa na  Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro.

Nafasi ya Katibu Organaizesheni amekuwa Mohamed Seif Khatibu, ambapo nafasi ya Uchumi na fedha imekwenda kwa Zakhia Hamdan Meghji.

Aliyewahi kuwa katibu Mkuu wa CCM,Philipo Mangula ambaye baada ya kustaafu alikuwa Mkulima ya Nyanya ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara, ambapo Rais wa Zanzibar, Dk.Shein amekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.

Monday, November 12, 2012

WAJUE WANEC 20 BARA NA ZANZIBAR NA KURA ZAO

DODOMA

Washindi wa Nec Bara,Stephen Wasira(2,135), January Makamba (2,093), Mwigulu Nchemba(2,010), Martine Shigela(1,824) na William Lukuvi(1,805).

Wengine ni Dk. Bernard Membe(1,455), Dk. David Mathayo(1,414), Wilson Mukama( 1,374), Jacksone Msome(1,207 na Dk. Fenella Mukangara(984).

Kwa upande wa Zanzibar walioshinda ni Dk. Makame mnyaa Mbarawa(1,850), Dk. Mohammed Seif Khatib(1,668), Khadija Hassan Aboud (1,625) na Shamshi Vuai Nahodha(1,603).

Wengine ni Dk. Hussein Ali Mwinyi(1,579), Samia Suluhu Hassan(1,525), Omary Yusuf Mzee(1,415), Banguaji Mansuria(1,406),Chasama(1,248) na Hamis Mbeto khamis (1,233).

Kwa matokeo haya inaonekana kuwa bado akina mama wako nyuma sana  kuthaminiana kutokana na mfumo dume ambao umezoeleka kwa Watanzania walio wengi, pamoja na kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. Jakaya Kikwete kutoa kipaumbele na kutoa nafasi nyingi kwa akina mama kushika nyadhifa mbalimbali katika uongozi wake wakiwemo Spika wa Bunge na Mawaziri 
 lakini wenyewe kwa wenyewe wamekuwa hawapeani kipaumbele kwa kile kinachodaiwa kutokuwa na Umoja.

WAJUE WAJUMBE WA WA NEC BARA WALIOJITOSHA VITI 10

Shy-Rose Bhanji nje Tena!












Tuesday, November 6, 2012

NANI MRITHI WA KIKWETE?

KWA KHERI DK. JAKAYA HALFAN MRISHO KIKWETE NOVEMBA 13 NDO MKUTANO WAKO WA MWISHO LABDA KUWEPO MABADILIKO YA KATIBA.

TUJIKUMBUSHE 2010:
JakayaKikwete2010




Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM,Jakaya Kikwete alipokutana na waandishi wa habari akinadi sera na kuzungumzia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2005/2010 ilivyotekelezwa katika kipindi alipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



Ucheshi wake Rais hautasahaulika kamwe! aliweza kuchati na wapiga kura wake kwa mtindo wa kidali po!! alitamani kuwashika watu wote mikono lakini alishindwa,waliobahatika kushika mkono wake wasema hawawezi kunawa Mkono huo ulioshikwa na Rais bali,watakula chakula bila kunawa,hii iliwahi kutokea katika kijiji cha Busekela Jimbo la Uchaguzi la Musoma Vijijini ambapo ilikuwa ni mara ya kwanza kufika hapo.
























Mwenyekiti Mstaafu,wa CCM na Rais wa awamu ya Tatu,Mh. Benjamin Mkapa akipeana Mkono na Mjumbe wa Halmashauri Kuu NEC,kwa sasa ndiye Makamu wa Rais, Dk.Mohamed Gharibu Bilal anayetabasamu katikati ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Ally Haji Ally Hassan Mwinyi (Mzee Ruksa) kabla ya kuanza kwa kampeni Jagwani jijini Dar es Salaam.

























Mgombea akinadi sera,katika tukio ambalo halitasahaulika katika kurasa za ubongo wa Mtanzania ni pale mgombea huyo alipoanguka,katika Uwanja huu wa jagwani, kwa kile kilichodaiwa kuwa ni uchovu pia mfungo,mgombea alikuwa amefunga, kipindi hiki kilikuwa kigumu kwa watanzania walio wengi kipenzi chao kuanguka ghafla.Pamoja na misukosuko yote kesho yake aliweza kuendelea na kampeni na afya yake ilikuwa njema.

Monday, November 5, 2012

JK AKAGUA UPANUZI WA WHITE HOUSE DODOMA

 DODOMA.

Rais Jakaya Kikwete amekagua upanuzi wa Ukumbi wa Mikutano katika Jengo la ofisi ya Mwenyekiti wa CCM (White House) Mkoa wa Dodoma.

Majira ya saa 10:15 Rais Kikwete na Mwenyekiti wa CCM,alikagua upanuzi na ukarabati wa jengo hilo ambapo linakaribia kumalizika.

Upanuzi huo unaofanywa na Mkandarasi toka China na wazalendo na ulianza kufanyiwa ukarabati mwanzoni mwa mwezi huu, ili kukidhi idadi ya wajumbe wa NEC ambapo kipindi hiki ni wengi.


Rais Kikwete pia amekagua  maendeleo ya maandalizi  ya Ukumbi wa Kizota unatarajiwa kufanyika Mkutano Mkuu wa CCM Oktoba 13.

Mkutano Mkuu wa CCM,pamoja na mambo mengine unatarajiwa kufanya Uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM,Makamu Wenyeviti wa CCM Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.


Pia Mkutano Mkutano Mkuu wa CCM utafanya Uchaguzi wa wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa viti 10 Bara na viti 10 Tanzania Zanzibar na kufanya marekebisho ya katiba ya CCM ya Mwaka 1077 Toleo 2010.

BALOZI WA MISRI AKIAGANA NA MAKAMU WA RAIS

MAKAMU wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Misri aliyemaliza muda wake nchini, WAEL Adel Nasr, Ikulu Dares Salaam.


UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM (JK)



RAIS JK akikagua chanzo cha maji katika halmashauri ya Mji wa Lindi, Kitunda kata ya Msinjahili, Agosti 22.

MTOTO WA MKULIMA AKIFUNGUA MAJENGO YA NHC







WAZIRI Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda, Agosti 17 alizindua ujenzi wa maghorofa ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Medeli Mjini Dodoma. Kushoto kwake ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka,kwa sasa Mji wa Dodoma unakua kwa kasi sana zaidi ya miji mingine kutokana na majengo mapya kuibuka haraka haraka,ndoto ya Dodoma kuwa Makao Makuu haswa sasa inaonekana kwa vitendo kuliko Mji ulivyokuwa hapo awali.