DODOMA.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM,Wilson Mukama ametolewa katika Uongozi huo na nafasi yake kuchukuliwa na Abdulahman Kinana.
Mukama ni Katibu Mkuu wa kwanza aliyewahi kukaa kwa muda mfupi,ambapo amedumu kwenye kiti kwa muda wa Mwaka Mmoja tu.
Habari kutoka hapa Dodoma zimesema kuwa katibu Mkuu huyo ametolewa kutokan ana kutokuwa mahiri katika kujibu hoja za wapinzani.
Naibu katibu Mkuu Bara, amekuwa Mwigulu Nchemba, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, amekuwa Ally Vuai ,Huku Nape Nnauye amebaki na nafasi yake ya Uenezi,huku nafasi ya January Makamba ya Mahusiano ya Nje ikichukuliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro.
Nafasi ya Katibu Organaizesheni amekuwa Mohamed Seif Khatibu, ambapo nafasi ya Uchumi na fedha imekwenda kwa Zakhia Hamdan Meghji.
Aliyewahi kuwa katibu Mkuu wa CCM,Philipo Mangula ambaye baada ya kustaafu alikuwa Mkulima ya Nyanya ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara, ambapo Rais wa Zanzibar, Dk.Shein amekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.
No comments:
Post a Comment