DODOMA.
Rais Jakaya
Kikwete amekagua upanuzi wa Ukumbi wa Mikutano katika Jengo la ofisi ya
Mwenyekiti wa CCM (White House) Mkoa wa Dodoma.
Majira ya saa 10:15 Rais Kikwete na Mwenyekiti wa CCM,alikagua upanuzi na ukarabati wa jengo hilo ambapo linakaribia kumalizika.
Upanuzi huo unaofanywa na Mkandarasi toka China na wazalendo na ulianza kufanyiwa ukarabati mwanzoni mwa mwezi huu, ili kukidhi idadi ya wajumbe wa NEC ambapo kipindi hiki ni wengi.
Rais Kikwete pia amekagua maendeleo ya maandalizi ya Ukumbi wa Kizota unatarajiwa kufanyika Mkutano Mkuu wa CCM Oktoba 13.
Mkutano Mkuu wa CCM,pamoja na mambo mengine unatarajiwa kufanya Uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM,Makamu Wenyeviti wa CCM Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.
Pia Mkutano Mkutano Mkuu wa CCM utafanya Uchaguzi wa wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa viti 10 Bara na viti 10 Tanzania Zanzibar na kufanya marekebisho ya katiba ya CCM ya Mwaka 1077 Toleo 2010.
No comments:
Post a Comment