MUSOMA
JESHI la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara limefanikiwa
kufanya ukaguzi wa tahadhari na kinga ya moto
katika Manispaa ya Musoma licha za zoezi hilo kuingiwa na dosari kwa
baadhi ya wamiiliki wa maduka kukataa kukaguliwa na kulipia ada ya Ukaguzi.
Akizungumza na
Uhuru ofisini kwake, Kaimu Kamishna Mkuu
wa Kikosi cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara Don Mhally alisema kuwa kwa upande wa Wilaya zingine
zoezi hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa lakini kwa Manispaa ya Musoma baadhi
ya wamiliki walikataa kwa kile kinachodaiwa kuwa utoaji wa fedha bila kupatiwa kifaa cha kuzimia
moto.
Alisema kuwa baadhi
ya wamiliki wa maduka waliokaa kukaguliwa wameachukuliwa sheria ikiwa ni pamoja
na kufikisha Mahakamani kwa kosa la kukiuka Sheria ya ya Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji Na.14 ya mwaka 2007 pamoja na kanuni zake za mwaka 2008(Fire Safety
Inspection and Certificate) na marekebisho yake ya mwaka 2012.
Jumla ya maduka ya kawaida zaidi ya 74 yamekaguliwa na
kulipia gharama ya ukaguzi na cheti na makusanyo ilikuwa ni sh.
54,590,000,ambapo kutoka Julai-Novemba 2012 jumla ya maeneo 431 yamekaguliwa na
zoezi hili ni la mwaka mzima wa fedha hadi Juni 30.
Aidha wametakiwa kuwa na kifaa cha kuzimia moto ambavyo
vinapatikana kwa mawakala walioteuliwa, aliwataja kuwa ni Sodobhi Investment,Dawill
Trading Agency(ZK) na Musoma Equipment Agency za Mjini hapa.