Tuesday, August 24, 2010
SHAMRASHAMRA JIMBONI BUSANDA
Mgombea Urais Jimbo la Busanda na Mgombea Ubunge pozi tofautitofauti
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa ndani ya helkopta kuelekwa kwenye msiba wa mtoto wa Mgombea Ubunge Jimbo la biharamulo mashariki Wilaya ya Chato, John Magufuri kwa maziko ambapo ziara yake ya kuelekea Buseresere Mkoa wa Kagera imehairishwa kutokana na msiba huo.
Mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM,Rais Jakaya Kikwete,akimshika bega kama ishara ya kumnadi Mgombea Ubunge jimbo la Busanda,Lolencia Bukwimba wakati amkimnadi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Katoro Geita Mkoani Mwanza.
Thursday, August 19, 2010
PICHA ZA WAGOMBEA MBALIMBALI WA MUSOMA MARA.
WAGOMBEA UBUNGE WA VYAMA VYA UPINZANI.
UREJESHAJI FOMU.
Wednesday, August 18, 2010
Katibu wa CCM Mkoa wa Mara, Ndeng’aso Ndekubali akimkabidhi na kumtambulisha kwa viongozi wa CCM wa Wilaya ya Tarime,Mgombea Ubunge Mteule wa Wilaya ya hiyo, Nyambari Chacha Nyangwine mara baada ya kuteuliwa na NEC,kabla ya kuanza kwa kikao cha Chama kilichofanyika katika ukumbi wa CCM Wilayani hapo jana.
Picha na Eva-Sweet Musiba.
Wagombea Ubunge wateule wa CCM wa Wilaya za Rorya na Tarime wakisikiliza kwa makini maagizo kutoka kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Mara, Ndeng’aso Ndekubali hayupo pichani wakati wa kikao cha Viongozi wa CCM wa Wilaya hizo wa kuwatambulisha viongozi waliopitishwa kuipeperesha vyema bendera ya CCM wa Ubunge, Udiwani na Udiwani wa viti Maalum katika hafla fupi iliyofanyiaka katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Tarime jana.
Katibu wa CCM Wilaya ya Rorya, Abubakar Ghati akimpokea Mgombea Ubunge Mteule wa Wilaya ya Rorya Lamek Airo,wakati wa utambulisho wa viongozi wateule wa Ubunge,Udiwani na Udiwani wa Viti Maalum Wilaya ya Tarime yaliyofanyika jana katika Ukumbi wa Wilaya katika yao ni Katibu wa CCM Mkoa wa Mara,Ndeng’aso Ndekubali.
Picha na Eva-Sweet Musiba.
Picha.Katibu Kikaoni.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mara, Ndeng’aso Ndekubali akisitiza jambo katika kikao cha Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM,kilichofanyika jana katika Ukumbi wa CCM Wilaya ya Tarime,kulia kwake ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo ,Rashid Mbogomba
Picha na Eva-Sweet Musiba.
Baadhi ya Madiwani wateule wataopambana na vyama vya upinzani kupeperusha bendera ya CCM Wilayani Tarime katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31 mwaka huu.
Picha na Eva-Sweet Musiba.
Viongozi wa CCM Mkoa wa Mara wakisali,baada ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mara,Ndeng’aso Ndekubali kutangaza kifo cha Mume wa aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu,Gaudentia Mgosi Kabaka na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, kilichotokea ghafla jana.
Monday, August 16, 2010
.
BAADHI ya wazazi wa watoto wanaosoma katika Shule ya Sekondari ya wasichana ya Chief Wanzagi iliyoko Butiama Mkoani Mara wamelalamikia uongozi wa Shule kuendeshwa kwa muda wa miaka mitatu bila ya kuwa na bodi ya shule jambo ambalo limekuwa likichangia migogoro Shuleni hapo ambapo zaidi ya Wanafunzi wapatao 100 wa kidato cha III katika shule hiyo wamefukuzwa shule kwa kosa la kuandamana usiku wa manane.
Shule hiyo pia kutokana na kutokuwa na bodi,pia kamati ya nidhamu hata baraza la wanafunzi wamekuwa wakishindwa wapi pa kupeleka malalamiko yao.
Katibu wa Askofu ambaye pia ni Askofu wa Kanisa Katoliki,Pius Jumapili na msaidizi wa Askofu,Julius Ogola walifika shuleni hapo kuangalia uzito wa suala hilo.
Kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya wanafunzi hao waliofukuzwa kwa kufanya maandamano hayo ili kwenda kuonana na askofu wa kanisa katoliki jimbo la Musoma Mjini Musoma ilikuwa ni kutoa malalamiko kwa Padri mmoja ambaye ni mwalimu katika shule hiyo kwa madai ya kuwalazimisha kufanya nao mapenzi ambapo wanafunzi wapatao watatu walitoa malalamiko yao hadharani na ndipo wenzake wakafanya uamuzi wa kuandamana ili wenzao warejeshwe masomoni.
Wanafunzi hao cha kidato cha tatu waligoma kula chakula cha mchana na kushinikiza wanafunzi hao warudishwe,ambapo mgomo huo haukusikilizwa .
Pamoja na Mgomo huo wamepewa wik i mbili wanafunzi hao wawe wamerudi na wazazi wao na ndipo maamuzi yatakapotolewa.
Wanafunzi hao waliofukuzwa ni kutoka maeneo mbalimbali ya nchi. kinyume cha sheria.
Walisema kuwa pamoja kutoa malalamiko kuhusu "kwanza tulikataa chakula kutwa nzima kushinikiza wenzetu watatu warudishwe shule na kuondolewa kwa huyo mwalimu lakini hakuna kilichofanyika ilitubidi sasa tuandamane saa nane usiku kwenda kuonana na uongozi wa jimbo kuelezea kilio chetu lakini tukiwa tumefika kilometa kama 40 hivi alikuja Padri Ogola na kuturudisha shuleni"alisema mmoja ya wanafunzi hao.
Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo sista Barbiana Brendony,alisema kuwa wanafunzi hao walifanya maandamano hayo usiku wa agosti 2 mwaka huu wakishiniza kurudishwa shuleni kwa wanafunzi wengine watatu ambao walifukuzwa shule kwa madai ya utovu wa nidhamu.
Adhabu iliyotolewa ni kuwarudisha nyumbani kwa muda wa wiki mbili na baada ya hapo kila mwanafunzi atakuja na mzazi wake kwa kujieleza na endapo wataridhika na maelezo yake wataendelea kuwa na mtoto wake.
Ujenzi wa shule hiyo ya kisasa ulianza kutekelezwa na Baba wa Taifa mwalimu Julius Nyerere na baada ya kufariki dunia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Nimrod Mkono aliendeleza ujenzi huo kama njia moja wapo ya kuenzi mchango wa kiongozi huyo kisha kukabidhiwa kanisa katoliki kuendesha.
MAPOKEZI YA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CHADEMA
WAGOMBEA UBUNGE WA MJINI MUSOMA KUPITIA CCM WALIOPELEKESHENA
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini Vedastus Mathayo Manyiyi akiwa amekaa akisubiri kupanda jukwaani kunadi sera zake wakati wa akura za maoni,eneo la Nyakato Mjini Musoma.Mathayo amepitishwa na NEC kuwa Mgombea Ubunge jimbo la Musoma Mjini,ambapo atapambana na vyama vya Upinzani kama Chadema ambapo Mgombea wake ni Mtoto wa Kaka yake Baba wa Taifa,Marehemu Kiboko Nyerere,Vicent Nyerere.
Mgombea Ubunge Jimbo la Musoma Mjini,Eliud Esseko Tongola(Mkorea) alipata nafasi ya pili kwa kura za maoni.Ni vyema kuwa amefanya maandalizi mazuri kwa ajili ya awamu ijayo.
Thursday, August 12, 2010
MAPENZI YAFANYA WAUANE HUKO MARA
MUSOMA
MWANAMKE mmoja amefariki Dunia kwa kuchomwa na kisu na mumewe sehemu mbalimbali mwilini kwa wivu wa mapenzi na mumewe pia kujiua kwa kujichoma kisu tumboni na utumbo kumwagika nje.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara,Robert Boaz aliwataja wapenzi hao kuwa ni Bageni chacha (28) na mumewe Juma Keresa (28) wote wakazi wa Mjini Wilaya ya Serengeti.
Tukio lilitokea juzi Agosti 11 majira ya saa 9:30 usiku mtaa wa Stend mpya mjini Mugumu ambapo mumewe baada ya kufanya kitendo hicho alijichoma kisu,ambapo alipelekwa katika hospitali ya Nyerere DDH ya mjini Mugumu na muda mfupi baadae alifariki dunia.
Katika tukio jingine mwanamke mmoja mwenye umri kati ya miaka 30 au 40 jana amekutwa amefariki dunia pembezoni katika ufweke wa ziwa Victoria,eneo la Lakeside Mjini Musoma majira ya saa 8:30 mchana na kifo chake hakijulikani.
Aidha wavuvi wawili pia wamekutwa wamefariki dunia na miili yao ikiwa imeharibika vibaya baada ya kufa maji,aliwataja wavuvi hao kuwa ni Kabichi Makongoro (32) na Mwikwabe Wisero(48/49) wote wakazi wa Nyarusulya wilaya ya Muoma Mjni.
Alisema kuwa wavuvi hao walikutwa majira ya saa 5 asubuhi Agosti 11 katika eneo la Lyamugasile, ambapo pia mtoto pacha alifariki dunia baada ya kuungulia kwenye nyumba ambapo watoto hao mapancha walikuwa wakichezea kibatari ambacho kililipuka na kuunguza godoro na moto kusambaa nyumba nzima.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara alimtaja Mtoto aliyefariki dunia kuwa ni Dotto Hamisi (7) mvulana ambapo Kurwa alipona katika janja hilo na kwamba wazazi hao hawakuwepo
Ikiwa ni siku ya nenda kwa Usalama barababari mtu mmoja mtembea kwa miguu alifariki dunia kwa kugongwa na gari katika barabara ya Bwai Mugando majira ya saa 1:30 .
Alimtaja aliyegogwa kuwa ni Nyamwenda Manumbu (60) na gari aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T 374 DJR ambapo dreva wa gari hilo alikimbia na jitihada za polisi kumtafuta zinafanywa.
Tukio jingine ni la Agosti 6 majira ya saa 12 za jioni katika eneo la Makutano Mjini hapa gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T 908 ADW lilimgonga mpanda baiskeli Masudi Sebastian (29) na abiria wake ambaye jina lake bado halijafahamika mwenye umri wa (30) wote wawili walifariki na chanzo cha ajali kinachunguzwa.
KURA ZA MAONI VITI MAALUM UWT MARA 2010
Rosemary Kirigini 288.
Agness Mathew 277
Kichena Chambiri 264
Nacy Msafiri 257
Rukia Wandwi 214
Francis Stella Sana 96
Veronica Nyerere 62
Evelyne Warioba 63
Norah Mkami 62
Lucy Malegeri 76
Caroline Nyerere 50
Jane Ngabo 48
Eva-Sweet Musiba ambaye ni Mwandishi wa habari vyombo vya CCM na mmiliki wa Blog hii alipata kura 40.
Consolata Maganga alipata kura 24.
Pamoja na kuwa washindi kwa nafasi ya tatu hadi ya tano,wagombea ubunge hao walipigwa chini kwa kutoweza kuingia katika kinyang'anyiro cha kapu Mjini Dodoma.
Wasomi wengi waliojitokeza katika kugombea Ubunge wa Viti Maalum Mkoani Mara walipuuzwa na kuchaguliwa wale ambao wana elimu ya chini.
kwa hili elimu kwa wapiga kura wetu itolewe si kuangalia pesa ya mtu kama ilivyokuwa katika uchaguzi huu.Pesa ilikuwa mbele kuliko uwezo na sera za mtu, na hata wajumbe kudiliki kuzomea baadhi ya wagombea.
NI KWELI ZITTO KABWE HATAKI TENA UBUNGE?
Inabidi Tanzania tufike wakati tusione viongozi fulani ndio lazima wawepo madarakani bali sheria na sera zetu zimfanye kila kiongozi kuweza kuongoza. Nahili kamwe halitaletwa na kiongozi bali wapiga kura wanaoelewa nini maana ya kura zao. Kila anayechukua form ya kuwa kiongozi pamoja na yote ana malengo yake binafsi, na kutuletea maendeleo ni mpaka pale malengo yake yatakapo intersect na shida za wananchi la sivyo kalabagaho tutalia sana. Sio vizuri nchi au taasisi au chama au wananchi kuwekeza nguvu zake zote kwa mtu mmoja au kwa kikundi cha watu bali kwa mfumo imara. Hivi ndivyo nchi zilizoendelea zimefanya kwani sera na mifumo yao imekuwa ndio dira ya kila kiongozi na uelewa wa wananchi wao ndio nguzo ya utawala uelewa wa waandishi wa habari kuelimisha umma umeifanya serikali na bunge zao kuwa imara na kutokuyumbishwa na upepo upitao.
Naona swala la Kabwe kuamua kuachia ngazi liwe ni maamuzi yake. nani anajua kwamba akilazimishwa kuendelea ataweza kutimiza wajibu wake, ni hatari sana kumlazimisha mtu ambaye tayari amechoka kazi husika, kwani kumlazimisha kubaki utendaji wake huwa unakuwa hafifu, mfano Raisi angekubali kujiuzulu kwa Dr. Idrisa rashid mazila anayotupatia sasa hivi tusinge yapata, hii ni kwasababu ameona thamani yake iko juu na hakuna mtanzania mwingine wa kushika kazi yake, sasa anatutenda.
Ni vyema mtu akisema libeneke limemshinda anaachia ngazi tumshukuru na tumwage kwa amani kwani hatujui kichwani kwake ana nini. Tuwe tayari kwa mabadiliko yenye manufaa na salama.
Naona ingekuwa vyema tukamkubalia Zitto akaachia siasa na kufanya anachokipenda, kwani ukisoma mistari yake yeye mwenyewe anaonyesha siasa za Tanzania zimemchosha/kumshinda kwani mara ya kwanza kasema anaachia ubunge na kwenda shule na kusaidia kukijenga chama kuanzia shina. hapo hapo kasema hana uzoefu wa uongozi hivyo atatafuta kwanza kazi ili apate uzoefu. hapo hapo kasema akimaliza shule tayari kaanza mipango ya kazi sudani au somalia.
Utajengaje chama wakati utakuwa masomoni na baada ya masomo unakwenda somali/sudani.
Pili je ni lini utapata huo uzoefu na je ni elimu ya kiwango gani anakihitaji je second degree or PHd na kama ni second ni miaka takribani miwili na sudan/somalia sijui miaka mingapi na kama ni PHd unaongelea miaka zaidi ya minne na sudan/somalia.
Ukiangalia vizuri Zitto is done on politics yeye awaage tu wapiga kura wake na aseme wazi nini kimemkuta ili awasaidie watanzania wengi vijana wenye mwelekeo wa kuingia dodoma mapema na asizungushe mbuyu, akumbuke ana haki ya kuwa au kutokuwa mbunge sio lazima na atashukururiwa kwa muda aliowatumikia watu wa Kigoma.
Monday, August 9, 2010
WIKI YA NENDA KWA USALAMA MKOANI MARA.
Akisoma risala kwa Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mara, Col. Enos Mfuru, Mkuu wa Kikosi cha Barabarani SP Mika Nyange kwa niaba ya Kamanda wa Kikosi cha Barabarani Mkoa wa Mara alisema jana kuwa mpaka sasa jumla ya Magari 1,695 yalikaguliwa na kati ya hayo makubwa ni 342,madogo 633 na pikikiki 720 kati ya hayo magari 1,687 yalionekana hayana makosa na magari manne yamefutiwa leseni.
Alisema kuwa ukaguzi huo husaidia kupunguza ajali barabarani kutokana n akuwepo kwa ongezeko la pikikpiki na baiskeli na watembea kwa miguu kutozingatia sheria za barababarani,ubovu wa barabara na hasa kwa kutofanyiwa matengenezo stahiki na kutokuwepo kwa alama za barabarani ni nyingine kung’olewa
Katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Mara Col. Enos Mfuru aligawa leseni na majaketi zaidi ya 60 ya kuakisi mwanga kwa wapanda pikipiki wa Wilaya ya Musoma Mjini kama ishara kuwa kuna usafiri wa pikikipiki hasa nyakati za usiku kwa usalama zaidi.
Akisoma Hotuba Mkuu wa Mkoa wa Mara alisema ili kukabiliana na aajali za barababani na kuepuka waendesha pikipiki,Taxi na magari makubwa hawana budi kuzingatia sheria za barababrni ili kuepukana na ajali zisizo za lazima ambazo zinahatarisha maisha ya wanadamu na wao wenyewe.
Kutokana na ajali za mara kwa mara kwa waendesha pikipiki na raia,Mkuu wa huyo wa Mkoa aliagiza Wakala wa barabara (TANROAD) Mkoa wa Mara kuweka matuta sehemu mbalimbali ambazo ajali hutokea mara kwa mara likiwemo barabara la Majita.
Madereva wa pikipiki wapatao 389 wamepewa mafunzo, na faini zilizotozwa kwa mwaka 2009 na 2010 kwa waliokiuka sheria walitozwa faini ya Sh. M.223,600.
Maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani kitaifa inafanyika Mkoani Tanga na kauli mbiu ni Ajali inaua, inajeruhi, usishabishe mwendo kasi,mpanda pikipiki vaa kofia ngumu.
Tuesday, August 3, 2010
MATOKEO YA UBUNGE MUSOMA VIJIJINI
1. BUSEE NASHON JI-DHABA'S 558
2. MARWA WAMBURA GEKONDO 363
3. MWITA JULIUS JOSEPH 237
4.ABEL MAIGA KAITIRA 224
5. NIMROD ELIREHEMA MKONO 34,113
6. PERE JOSHUA MUGANDA 167
7.SAMWEL MARERO MAGERO 119
8. ANTONY MTAKA 5,940
9. CHRISTOPHER MARWA SIAGI 1,700
10. BARAKA IMANYI OBAMA 408
MASIKINI KULIOINA BUNGE PIA NI "NDOTO" NINI CHA KUFANYA WEWE NA MIMI TOA MAONI.
ORODHA YA WAGOMBEA UBUNGE MUSOMA MJINI
ORODHA YA WAGOMBEA UBUNGE KURA ZA MAONI JIMBO LA MUSOMA MJINI.
1. NDUGU DEUS MUNASA SABI KURA ALIZOPATA 407
2. NDUGU ELIUD ESEKO TONGORA 3771 Mshindi wa pili
3. NDUGU ENOCK MWITA CHAMBIRI 1250 Mshindi wa Tatu
4. NDUGU FELISTA VITUS MRUSHA 312
5. NDUGU JULIUS HENRY LESHA 161
6 NDUGU JOHN KYABWE BWANA 69
7. NDUGU MAGORO MGALANI ALPHONCE 163
8. NDUGU VEDASTUS MATHAYO MANYINYI 6,489 Mshindi wa Kwanza.
9 NDUGU ZERULIA ZAKY MANENO 74
KURA ZILIZOPIGWA 13,546
KURA ZILIZOHARIBIKA 850
KURA HALALI 12,696
KATIBU WA CCM WILAYA YA MUSOMA MJINI ALIYETANGAZA MATOKEO MAMA HAULA KACHWAMBA.
Kuna uwezekano wa walioshindwa kwenda upinzani ama wakiunga Mkono wagombea wa katika kambi ya Upinzani kutoka na malalmiko yaliyopo na Vijana wengi waliojitokeza na kujiunga na CCM kwa ajili ya kuchagua wanayemwona anafaa watarejesha kadi za CCM kwa kambi za upinzani pindi tu kampeni zitakapoanza.
WAGOMBEA UBUNGE UWT WALALAMIKA.
Baadhi ya wagombea Ubunge Viti Maalum kundi la Wanawake walioshindwa katika kura za maoni za kuwapata wagombea watano kwa kila Mkoa,Mkoa wa Mara kupitia Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) wameliomba Baraza Kuu la UWT Taifa kuwachunguza baadhi ya wagombea waliopita katika Kura za maoni kabla ya kupendekeza ya majina yatakayowasilishwa kwa Halmashauri Kuu ya Taifa kutokana na ukiukwaji wa Kanuni.
Walisema kutokana na ukiukwaji huo,baadhi yao hawana sifa ya kuwa viongozi kwa kuwa si wanachama halali wa UWT kwani kifungu cha kanuni cha UWT kinasema Mwanachama atakayechukua fomu ya kugombea ni yule ambaye ni Mwanachama wa UWT kwa kipindi kisichopungua miaka Mitano.
Aidha walilamikia kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha ili kuhakikisha wanapitishwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa kinyume na Sheria ya Uchaguzi.
Wengine walivunja kanuni kwa kuwalaza wajumbe kwenye mahoteli siku moja kabla ya Uchaguzi.huku wakitaja Nyumba ya kulala wageni ya Toto’s ya Mjini Tarime kwa wajumbe wapatao 24 kabla ya Uchaguzi ,Mujungu Guest House ya Mjini Musoma.
Pia Uchunguzi uliofanywa na Mwandishi wa Habari hii umeonyesha kuwa ni vigumu kutekeleza Sheria kutokana na mazoea ya wanachama ambao wengi wao bila kuwapatia fedha hawawezi kuchagua kiongozi wanayemwona ni bora, bali bora kiongozi.
Wagombea Ubunge kundi la wanawake waliopitishwa kuingia tano bora Mkoani Mara ni Gaudentia Kabaka,Rosemary kirigini, Aggnes Mathew,Kichena Chambiri na Nancy Msafiri ambaye ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mara.