Monday, August 16, 2010

.

MUSOMA


BAADHI ya wazazi wa watoto wanaosoma katika Shule ya Sekondari ya wasichana ya Chief Wanzagi iliyoko Butiama Mkoani Mara wamelalamikia uongozi wa Shule kuendeshwa kwa muda wa miaka mitatu bila ya kuwa na bodi ya shule jambo ambalo limekuwa likichangia migogoro Shuleni hapo ambapo zaidi ya Wanafunzi wapatao 100 wa kidato cha III katika shule hiyo wamefukuzwa shule kwa kosa la kuandamana usiku wa manane.

Shule hiyo pia kutokana na kutokuwa na bodi,pia kamati ya nidhamu hata baraza la wanafunzi wamekuwa wakishindwa wapi pa kupeleka malalamiko yao.

Katibu wa Askofu ambaye pia ni Askofu wa Kanisa Katoliki,Pius Jumapili na msaidizi wa Askofu,Julius Ogola walifika shuleni hapo kuangalia uzito wa suala hilo.

Kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya wanafunzi hao waliofukuzwa kwa kufanya maandamano hayo ili kwenda kuonana na askofu wa kanisa katoliki jimbo la Musoma Mjini Musoma ilikuwa ni kutoa malalamiko kwa Padri mmoja ambaye ni mwalimu katika shule hiyo kwa madai ya kuwalazimisha kufanya nao mapenzi ambapo wanafunzi wapatao watatu walitoa malalamiko yao hadharani na ndipo wenzake wakafanya uamuzi wa kuandamana ili wenzao warejeshwe masomoni.

Wanafunzi hao cha kidato cha tatu waligoma kula chakula cha mchana na kushinikiza wanafunzi hao warudishwe,ambapo mgomo huo haukusikilizwa .

Pamoja na Mgomo huo wamepewa wik i mbili wanafunzi hao wawe wamerudi na wazazi wao na ndipo maamuzi yatakapotolewa.

Wanafunzi hao waliofukuzwa ni kutoka maeneo mbalimbali ya nchi. kinyume cha sheria.

Walisema kuwa pamoja kutoa malalamiko kuhusu "kwanza tulikataa chakula kutwa nzima kushinikiza wenzetu watatu warudishwe shule na kuondolewa kwa huyo mwalimu lakini hakuna kilichofanyika ilitubidi sasa tuandamane saa nane usiku kwenda kuonana na uongozi wa jimbo kuelezea kilio chetu lakini tukiwa tumefika kilometa kama 40 hivi alikuja Padri Ogola na kuturudisha shuleni"alisema mmoja ya wanafunzi hao.

Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo sista Barbiana Brendony,alisema kuwa wanafunzi hao walifanya maandamano hayo usiku wa agosti 2 mwaka huu wakishiniza kurudishwa shuleni kwa wanafunzi wengine watatu ambao walifukuzwa shule kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Adhabu iliyotolewa ni kuwarudisha nyumbani kwa muda wa wiki mbili na baada ya hapo kila mwanafunzi atakuja na mzazi wake kwa kujieleza na endapo wataridhika na maelezo yake wataendelea kuwa na mtoto wake.

Ujenzi wa shule hiyo ya kisasa ulianza kutekelezwa na Baba wa Taifa mwalimu Julius Nyerere na baada ya kufariki dunia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Nimrod Mkono aliendeleza ujenzi huo kama njia moja wapo ya kuenzi mchango wa kiongozi huyo kisha kukabidhiwa kanisa katoliki kuendesha.


1 comment:

  1. Sweet, you must be posting news here on your blogsite in one hell of real hurry. There's nothing infuriating to a reader than the numerous spelling errors, incomplete stories, missing or wrong names and pictures that your blog is laden with. In fact, I was surfing for Musoma news and I got here. Turn this blog into a more interesting site and you will have plenty of repeating visits. I will be visiting in two weeks and I hope you will have put in more effort to improve your blog. Otherwise, we wish you well.

    ReplyDelete