Thursday, August 12, 2010

MAPENZI YAFANYA WAUANE HUKO MARA

VIFO KIBAO WIKI HII MKOANI MARA.

MUSOMA

MWANAMKE mmoja amefariki Dunia kwa kuchomwa na kisu na mumewe sehemu mbalimbali mwilini kwa wivu wa mapenzi na mumewe pia kujiua kwa kujichoma kisu tumboni na utumbo kumwagika nje.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara,Robert Boaz aliwataja wapenzi hao kuwa ni Bageni chacha (28) na mumewe Juma Keresa (28) wote wakazi wa Mjini Wilaya ya Serengeti.

Tukio lilitokea juzi Agosti 11 majira ya saa 9:30 usiku mtaa wa Stend mpya mjini Mugumu ambapo mumewe baada ya kufanya kitendo hicho alijichoma kisu,ambapo alipelekwa katika hospitali ya Nyerere DDH ya mjini Mugumu na muda mfupi baadae alifariki dunia.

Katika tukio jingine mwanamke mmoja mwenye umri kati ya miaka 30 au 40 jana amekutwa amefariki dunia pembezoni katika ufweke wa ziwa Victoria,eneo la Lakeside Mjini Musoma majira ya saa 8:30 mchana na kifo chake hakijulikani.
Aidha wavuvi wawili pia wamekutwa wamefariki dunia na miili yao ikiwa imeharibika vibaya baada ya kufa maji,aliwataja wavuvi hao kuwa ni Kabichi Makongoro (32) na Mwikwabe Wisero(48/49) wote wakazi wa Nyarusulya wilaya ya Muoma Mjni.

Alisema kuwa wavuvi hao walikutwa majira ya saa 5 asubuhi Agosti 11 katika eneo la Lyamugasile, ambapo pia mtoto pacha alifariki dunia baada ya kuungulia kwenye nyumba ambapo watoto hao mapancha walikuwa wakichezea kibatari ambacho kililipuka na kuunguza godoro na moto kusambaa nyumba nzima.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara alimtaja Mtoto aliyefariki dunia kuwa ni Dotto Hamisi (7) mvulana ambapo Kurwa alipona katika janja hilo na kwamba wazazi hao hawakuwepo
Ikiwa ni siku ya nenda kwa Usalama barababari mtu mmoja mtembea kwa miguu alifariki dunia kwa kugongwa na gari katika barabara ya Bwai Mugando majira ya saa 1:30 .

Alimtaja aliyegogwa kuwa ni Nyamwenda Manumbu (60) na gari aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T 374 DJR ambapo dreva wa gari hilo alikimbia na jitihada za polisi kumtafuta zinafanywa.

Tukio jingine ni la Agosti 6 majira ya saa 12 za jioni katika eneo la Makutano Mjini hapa gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T 908 ADW lilimgonga mpanda baiskeli Masudi Sebastian (29) na abiria wake ambaye jina lake bado halijafahamika mwenye umri wa (30) wote wawili walifariki na chanzo cha ajali kinachunguzwa.

No comments:

Post a Comment