JUMLA ya watu 86 wamefariki dunia kati ya mwaka 2009 na 2010 kwa ajali za barabarani Mkoani Mara na 318 kujeruhiwa na idadi ya waliokamatwa na makosa madogo madogo ikiwa ni 14068.
Akisoma risala kwa Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mara, Col. Enos Mfuru, Mkuu wa Kikosi cha Barabarani SP Mika Nyange kwa niaba ya Kamanda wa Kikosi cha Barabarani Mkoa wa Mara alisema jana kuwa mpaka sasa jumla ya Magari 1,695 yalikaguliwa na kati ya hayo makubwa ni 342,madogo 633 na pikikiki 720 kati ya hayo magari 1,687 yalionekana hayana makosa na magari manne yamefutiwa leseni.
Alisema kuwa ukaguzi huo husaidia kupunguza ajali barabarani kutokana n akuwepo kwa ongezeko la pikikpiki na baiskeli na watembea kwa miguu kutozingatia sheria za barababarani,ubovu wa barabara na hasa kwa kutofanyiwa matengenezo stahiki na kutokuwepo kwa alama za barabarani ni nyingine kung’olewa
Katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Mara Col. Enos Mfuru aligawa leseni na majaketi zaidi ya 60 ya kuakisi mwanga kwa wapanda pikipiki wa Wilaya ya Musoma Mjini kama ishara kuwa kuna usafiri wa pikikipiki hasa nyakati za usiku kwa usalama zaidi.
Akisoma Hotuba Mkuu wa Mkoa wa Mara alisema ili kukabiliana na aajali za barababani na kuepuka waendesha pikipiki,Taxi na magari makubwa hawana budi kuzingatia sheria za barababrni ili kuepukana na ajali zisizo za lazima ambazo zinahatarisha maisha ya wanadamu na wao wenyewe.
Kutokana na ajali za mara kwa mara kwa waendesha pikipiki na raia,Mkuu wa huyo wa Mkoa aliagiza Wakala wa barabara (TANROAD) Mkoa wa Mara kuweka matuta sehemu mbalimbali ambazo ajali hutokea mara kwa mara likiwemo barabara la Majita.
Madereva wa pikipiki wapatao 389 wamepewa mafunzo, na faini zilizotozwa kwa mwaka 2009 na 2010 kwa waliokiuka sheria walitozwa faini ya Sh. M.223,600.
Maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani kitaifa inafanyika Mkoani Tanga na kauli mbiu ni Ajali inaua, inajeruhi, usishabishe mwendo kasi,mpanda pikipiki vaa kofia ngumu.
No comments:
Post a Comment