Monday, September 12, 2011

MKOA YA KANDA YA ZIWA MVUA NI NYINGI(KILIMO KIANZE)

MIKOA ya Kanda ya ziwa hapa nchini imetajwa kuwa inaoongoza kwa kupata mvua mara mbili kwa kipindi cha mwaka 2011 kufuatia tathimini ya mvua za msimu kwa miezi ya Machi na Mei.



Akizungumza na waandishi wa habari mjini Musoma Meneja wa mamlaka ya hali ya hewa Mkoa wa Mara,Bw. Mkono amesema kuwa baadhi ya maeneo yanapata mvua za wastani ambapo Mkoa wa Manyara ,Dodoma ,Singida ,Tabora, Shinyanga na Kaskazini mwa mkoa wa Kigoma yalipata mvua chini ya wastani pamoja na maeneo ya Pwani ya Kaskazini mkoa wa pwani ,visiwa vya unguja na pemba.



Amesema kuwa baadhi ya maeneo ya nyanda za juu kusini Magharibi Mikoa ya Mbeya na Iringa yalipata mvua za juu ya wastani ambapo maeneo machache yalipata mvua za juu ya wastani na kufanya mtawanyiko wa mvua hizo kutoridhisha.


Ameongeza kuwa kwa Mikoa ya kanda ya ziwa Mkoa wa Mara unaongoza kwa kuwa na mvua nyingi kwa kiwango cha wastani wa 534.9 milimita sawa na asilimia 132 ikifuatiwa na Mkoa wa Kagera na Shinyanga.



Amesema Mikoa inayofuata kwa wingi wa mvua ni Nyanda za juu Kaskazini Mashariki,pwani ya Kaskazini,Nyanda ya Kaskazini Magharibi ,Pwani ya Kusini,Kanda ya Kati na kanda ya kusini.

Viwango vya mvua chini ya asilimia 75 chini ya wastani kwa kipindi kirefu utafasiliwa kama chini ya wastani,wakati viwango vya kati ya asilimia 75 hadi 125 kutofasiliwa kama mvua za wastani na zile za zaidi ya asilimia 75 kama juu ya wastani.



Bw. Mkono amewashauri wakulima kutumia msimu huo wa mvua kulima mazao mbalimbali ili kukabiliana na janga la njaa linaloikumba nchi pamoja na mfumko wa bei za vyakula unaopanda mara kwa mara.



Hata hivyo utabiri wa hali ya hewa kutoka makao makuu unatabiri kuwa mwezi Oktoba mwaka huu kuwa na mafuriko, hivyo Mikoa ya kanda ya ziwa hasa Mwanza ambapo kumewahi kutokea mafuriko mwaka 1999 na kupoteza maisha ya mamia ya wakazi, ikiwemo upotevu wa mifugo na mali za wananchi yaliyoadhirka hasa maeneo ya mabatini na wakazi wengine wanaoishi bondeni,ambapo Waziri Mkuu wa kipindi hicho Fredrick

Sumaye alipiga marufuku ujenzi wa watu wanaoishi kando kando yam to Mirongo ambao unatirirsha maji kwa wingi kutoka Milimani na kwenda ziwani.


No comments:

Post a Comment