Tuesday, September 20, 2011

WAZIRI MKUU AIMWAGIA SIFA WILAYA YA SERENGETI

SERENGETI.

WAZIRI MKUU,Mizengo Pinda ameipongeza Wilaya ya Serengeri kwa kuwa na miradi yenye tija na kuwataka kuongeza mizinga ya asali kutoka 50 hadi 500 ambalo litakuwa shamba darasa.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mbuzi katika Wilaya ya Serengeti Waziri Mkuu alisema kuwa kati ya Wilaya ambazo alitembelea Wilaya hiyo imefanya jitihada kubwa kuhakikisha wananchi wanapata manufaa na kupata kipato chao binafsi.

Miradi aliyoikagua na kuweka jiwe la msingi ni pamoja na mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya chumba cha (mapokezi na chumba cha upasuaji),mradi wa lambo wa kijiji cha Nyamisingisi, mradi wa maji wa bwawa la Mugumu( Manchira) na mradi wa ujenzi wa bweni shule ya sekondari Ikoma.
Mradi wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ulikadiriwa kutumia jumla y ash. Bilioni 13 kwa bei ya mwaka 2008,kutokana na ukubwa wa gharama za mra huo kiasi kidogo cha fedhadi kilichokuwepo kwa ajili ya kuanza utekelezaji Tsh. 761,530,000, mtaalamu alishauri kuwa mradi huo utekelezwe kwa awamu mbili,ambapo awamu ya kwanza ilihusisha ujenzi wa msingi na kuta hadi kufikia usawa wa lenta(RingBeam) na awamu ya pili itahusisha ukamilishaji wa jengo lote ambalo kwa sasa limekwama.
Jengo la upasuaji ambalo limepauliwa na kupigwa lipu ndani na nje ,kuwekwa mbao na signboard(blunderling) lililowekwa jiwe la msingi la Waziri Mkuu,litatumia Sh. 488,893,700 ambapo hadi sasa limegharimu jumla ya Sh. 213,988,505.
Mradi wa Lambo la kijiji cha Nyamisingisi ,bilika la kunyeshea mifugo na kituo cha kuchotea maji ni kati ya miundo mbinu ya maji na usafi wa mazingira katika mradi wa ‘Maji ni Uhai’unaotekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la AMREF kwa kushirikiana na halmashauri,ukifadhiliwa na kampuni ya ujenzi wa Ferrovial toka nchini Japan umegharimu Tsh. 2,305,508,000 ambapo mfadhili ametoa Tsh. 2,240,000,000 na mchango wa wananchi ni Tsh. 65,580,000.
Kutokana na kukamilika kwa mradi wa Bwawa la maji la Manchira kumejitokeza shughuli zingine ndani ya bwawa na kuzunguka eneo la bwawa ikiwa ni pamoja na ufugaji wa samaki, ufugaji wa nyuki na uhifadhi wa misitu na wanyamapori.
Aidha zoezi la ufugaji wa samaki katika bwawa la Mugumu ulianza baada ya kukamilika ujenzi wa bwawa mnamo mwaka 2009 kwa kupandikiza vifaranga vya samaki 15,000 aina ya sato( Tilapia) ambao walipatikana kutoka kituo cha utafiti wa uvuvi (TAFIRI) Sota, Wilaya ya Rorya,ambao zoezi la kuanza kuwavua kwa majaribio umeanza na samaki watarajiwa kuanza kuuzwa kwa Sh. 1000-1500.

Mradi wa ujenzi wa bweni la wavulana katika sekondari kwa ajili ya kidato cha tano na sita iliyojegwa kupitia mradi wa TASAF kwa gharama ya Sh. 59,000,000,nguvu za wananchi sh. Milioni 9 na mchango wa TASAF Tsh. 49,000,000,ambapo zinajumuisha ujenzi wa bweni, choo, na bafu, utengenezaji wa vitanda double decker 24 na ununuzi wa magodoro 48.

Akisoma risala kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda Mkuu wa Shule hiyo, Sabina Mwishauri alisema changamoto zinazoikabili shule hiyo ni pamoja na ukosefu wa umeme wa gridi ya Taifa ambao upo umbali wa mita 800 kutoka kwenye trasfoma kwenda shuleni hapo ambao unagharimu jumla ya Sh. Milioni 90.

No comments:

Post a Comment