Friday, September 23, 2011

SERIKALI KUTAIFISHA SUKARI ILIYOKAMATWA

MUSOMA.

SERIKALI imeagiza kutaifishwa kwa sukari yote iliyokamatwa Tarime mkoani Mara ambayo ilikuwa ikisafirishwa kwenda Kenya.


oparesheni maalum ya kuzuia magendo ya sukari iliyoanza septemba 21 Mkoani Mara baada ya agizo la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jumla ya mifuko 1,655 ya sukari imekamata.

“Nimeagiza sukari hiyo tuibebe, twende uwanjani, tuiuze kwa bei tunayojua sisi tuone anayelalamika ni nani…iuzwe kwa kila mmoja.

“Polisi msiwachekee wala msishirikiane nao (wavusha sukari), nimeambiwa kwamba kuna vizuizi vingi barabarani ambavyo havina tija vinalalamikiwa, tutaliona hilo,” alisema.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Robert Boaz baada ya kikao cha majumuisho kilichofanyika aktika ukumbi wa uwekezaji Mjini Musoma, inasema malori hayo yamekamatwa mpakani mwa Kenya yakielekea Tarime na Sirari.



Malori hayo yenye namba za usajili T.335 BPF aina ya fuso ilikuwa na mifuko 310, T.445 AWB aina ya fuso ilikuwa ina mifuko 310 mali ya mfanyabishara wa Tarime na Sirari, Josephat Wambura.


Nyingine ni namba T.695 ANE aina ya Scania iliyokuwa na maifuko 450 mali ya Ongujo Wakbar wa Mji mdogo wa Shirati na T.652 BGR aina ya Fuso mali ya Kuchikuchi wa Mjini Tarime.



Alisema kuwa uchunguzi unaendelea wa kubaini kama bidhaa hiyo imekusudiwa kutumika ndani ya nchi na kama sheria za nchi hazijavunjwa na wamiliki wa mali hizo.
Operesheni hiyo imefanyika baada ya Waziri Mkuu kupewa taarifa hizo na wananchi kulalamika katika mikutano mbalimbali ya hadhara alipokuwa na ziara yake Mkoani Mara iliyomalizika jana, juu ya kuwepo kwa baadhi ya askari kuvusha sukari kwenda nje ya nchi huku watanzania wakitaabika.

No comments:

Post a Comment