Sunday, September 25, 2011

RAIS KIKWETE KUWASHA UMEME MKOA MPYA SIMIU

NA SELEMAN BITALA
MWANZA.

RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwasha umeme jimbo la uchaguzi la kisesa wilayani Meatu mkoani Shinyanga Disemba mwaka huu.


Mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni kamishina wa vyuo vikuu na Mbunge wa Bunge la Afrika Mpina Luhaga amesema mradi huo utagharimu shilingi bilioini 1.6 na tayari nguzo zimeshasimikwa jimboni kote.



Katika juhudi za kuharakisha maendeleo mbunge amenuia kusogeza huduma za kibenki na polisi katika mji wa Mwandoya nao kwa sasa wananchi wanalazimika kusafiri kilomita 15 kupata huduma za usalama wa raia na mali zao wanapovamiwa na kuuawa na wezi wa mifugo.



kwa upande wa barabara tayari shilingi bilioni 1.5 zimetumika kujenga madaraja sasa tunashirikiana na Tanroad kutafuta mkandarasi anayestahili kufanya ujenzi wa mtandao imara wa barabara jimboni maana serikali imeshatoa pesa.” Mpina.

Ili kuwatumikia wapiga kura wake kwenye mkoa huo mpya wa Simiyu mbunge huyo anatumia fursa, kipaji na talanta kuleta maendeleo,vijiji vya Isangijo, Sakasaka, Matale, Buturi, Ingeke pia Mwang’hongo vilivyokuwa na mazingira hatarishi vimeboreka.


Licha ya mtandao wa barabara ambao ni muhimu kwa mazao ya wakulima pia amefanya mazungumzo na baadhi ya makampuni ya simu yatakayosogeza huduma zao pindi umeme ukiwapo lakini hivi sasa wananchi hao wanalazimika kupanda juu ya miti ili kukamata mtandao wa Airtel.


Kuhusu njaa iliyotokana na ukame imeelezwa serikali inatoa chakula cha misaada katika kila kipindi cha miezi mitatu.



Kwa zao la pamba ambalo bei yake kutoka kwa wanunuzi binafsi ilikuwa imeshushwa hadi kati ya shilingi 600 na 800 hali iliyomfanya ashiriki kupiga debe kiasi kwamba sasa imefikia 1,100 ili kilimo cha zao hilo kisiachwe na wakulima ambao bado wanataka ifikie sh. 1,500 wakiiomba serikali msaada wa kupatiwa pembejeo za kilimo.

No comments:

Post a Comment