Sunday, September 18, 2011

MUSOMA VIJIJINI NJAA HAKUNA TENA -PINDA

Ghati Msamba wa Uhuru

MUSOMA.

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amesema Mkoa wa Mara hauna sababu ya kuwa na njaa kutokana na mahindi ya Msaada ambayo yatawasili wiki hii Wilaya Musoma Vijijini.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Maneke na Murangi (MAJITA) Musoma vijijiji amesema tatizo lililopo ni ucheleweshwa wa mahindi hayo kutoka Mkoani Shinyanga na kufika katika maeneo huska.

Wananchi hao walipata mahindi ya msaada kwa awamu ya kwanza, hali hii ya kuwa na njaa katika vijijini takribani zaidi ya 50 inatokana na mihogo kuwa na ugonjwa wa batobato unaokula mizizi ambayo inazalisha mihogo na Muhogo wenyewe kuoza.

Akizungumzia juu ya ugonjwa huo aliagiza Wizara huska kuhakikisha inapeleka wataalamu ili kuhakikisha kuwa ugojwa huo unateketezwa pamoja na kuleta mbegu bora inayoweza kumudu magonjwa.

Vijiji ambavyo vina hali mbaya ya chakula ni pamoja Wanyere, Murangi, Chumwi, Rusoli, Busekela, Suguti, Kwikuba,na vingine vingi.

Wanananchi hao walitoa vilio vyao ikiwa ni pamoja na kutokuwa na barabara ya kiwango cha rami ambayo Rais Jakaya Kikwete alihaidi kuwa ya kiwango cha lami, Maji na umeme.

Akijibu hoja zao alisema kuwa kwa kuwa Rais aliishatamka hilo kwake ni kazi rahisi ya utekelezaji na si kusubiri.

Waziri Mkuu aliweka jiwe la Msingi,chumba cha upasuaji katika zahanati ya Murangi inayotarajiwa kupanuliwa na kuwa ya Wilaya ili iweze kukidhi matarajio ya wananchi.

Akiwa nyumbani kwa baba wa Taifa, aliweka shada la maua na kusali katika kaburi lake, na baadae akipata fursa ya kuzungumza na wananchi ambao walikuwa na shahuku juu ya ya Makao Makuu ya Wilaya ya Butiama kuwa kati ya Nyamisisi na Butiama.

Alipata fursa pia ya kuzungumza na familia ya baba wa Taifa,ambapo alizungumza na mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere na kijana wake Emily Magige kwa faragha.

Waziri Mkuu alikwenda kuangalia kituo cha uzalishaji wa mbegu bora ya Ng’ombe(Butima Artificial Insemination Center) kituo ambapo kinahitaji ukarabati wa hali ya juu ili kiweze kuanza kazi.

Anaendelea na ziara katika Wilaya za Bunda, Serengeti, Tarime na Rorya.

No comments:

Post a Comment