WAZIRI MKUU,Mizengo Kayanza Peter Pinda amewasili leo majira ya 12 katika uwanja wa ndege wa Musoma na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa.
Waziri Mkuu atakuwa na ziara ya siku saba akikagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Waziri Mkuu amepokea taarifa za serikali, Mkoa na Wilaya Ikulu ndogo majira ya saa 12 45.
Septemba 17 atapokea taarifa ya CCM kutoka kwa Katibu wa Chama, Ndekubali Ndengaso,pia atatembelea Shule ya msingi Mwisenge na darasa alilosomea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Atatembelea kiwanda cha nguo cha Mutex,Zahanati ya A.IC.T iliyoko Bweri na kuifungua na baadae atafanya Mkutano wa hadhara katika viwanja vya Mukendo Mjini Musoma.
No comments:
Post a Comment