Monday, September 12, 2011

RPC MWANZA ADANGANYA NI JUU YA KIFO CHA MWANDISHI

“PRESS RELEASE”

TAREHE 09/09/2011

TAARIFA YA KIFO CHA MAREHEMU

RICHARD S/O MASATU

Mnamo tarehe 08/08/2011 majira ya saa nne na nusu ukiku huko Igoma (W) Nyamagana jijini Mwanza, RICHARD S/O MASATU, ambaye kwa sasa ni marehemu mika 39 Mjita na aliyekuwa Mkurugenzi wa gazeti la Kasi Mpya la Jijini Mwanza, mkazi wa Nyakato aliokotwa eneo la barabara kuu itokayo Mwanza kwenda Musoma akiwa na majeraha.

Majeruhi alikutwa hatua chache toka eneo la Namda bar/hotel barabara iendayo Musoma kutoka Mwanza.

Kama nilivyokuwa nimewahaidi toka mwanzo kuhusiana na tukio hili upelelezi wa kina umeendelea kufanyika. Upelelezi tuliofanya umeonyesha kwamba majeruhi alotolewa eneo la tukio akiwa mzima na aliweza kuongea na watu wachache waliompa msaada wa kufikishwa hospitali ya Sekou-toure kwa matibabu ambako pia mke wake alimkuta akiwa hai. Majeruhi alifariki baada ya siku mbili tangu siku ya tukio yaani tarehe 10/08/2011 majira ya saa nane usiku. KAtika upelelezi/ushahidi uliokusanywa mpaka sasa unaonyesha kwamba marehemu RICHARD S/O MASATU aligongwa na gari ambalo halikuweza kufahamika aina, rangi wala namba zake za usajili.

Tumefanikiwa kupata na kuwahoji watu walioshuhudia tukio hilo la ajali muda mchache baada ya kutokea ni pamoja na shuhuda aliyeombwa na marehemu [wakati akiwa bado hai] kwamba amwokoe na kwamba alikuwa amepata ajali.

Majeraha aliypata marehemu katika ajali hiyo ni kama yafuatayo:-

1. Michubuko kwenye mguu wa kushoto

2. Mvunjiko wa ndani mguu wa kushoto

3. Michubuko na majeraha upande wa kulia wa paji la uso

4. Michubuko katika mkono wa kulia na kushoto

5. Alipasuka bandama na pia alipata majeraha makubwa sehemu ya kichwa.

Kesi iliyobaki kwetu ni kuongeza juhudi za kuipata gari lililosababisha kifo hiki ili tuweze kumuhoji na kumfikisha mtuhumiwa mbele ya sheria.

RAI

Ninatoa wito kwa wananchi wenye mapenzi mema ambao wanaweza wakawa na taarifa za tukio hili lililopelekea kifo cha marehemu RICHARD S/O MASATU zikiwemo za gari lililomgonga. Pamoja na utalaamu wetu katika upelelezi, wananchi wanayo nafasi kubwa sana kulishirikisha Jeshi juu ya taarifa mwanana za kihalifu na wahalifu.

(LIBERATUS BARLOW – ACP)

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

1 comment: