Monday, September 26, 2011

PLAN INTENATIONAL YASAIDIA WAJASILIAMALI

MWANZA.


Wanachama kutoka nchi mbalimbali za Afrika na Amerika wanakutana leo katika semina ya majadiliano juu ya maendeleo ya Tanzania na wajasiliamali mbalimbali kwa lengo la kujifunza nini Tanzania inafanya hususani katika Miji ya Mwanza,Mkoa Mpya wa Geita na Kisarawe yanayofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Malaika Beach Resort ya Jijini Mwanza.


Akifungua semina hiyo, Mkurugenzi Mkazi nchini ( Country Coordinator), David Muthungu alisema semina hiyo ya siku tatu ina lenga kuwaelemisha wanachama hao mbinu iliyotumika ya shirika hilo kuwasaidia wafanyabiashara ndogo ndogo jinsi ya kutunza fedha na kuzitumia vyema.


Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa semina hiyo, Muthungu alisema mafunzo hayo yanashirikisha washirika kutoka nchi za Tanzania ambao ndio wenyeji, Kenya, Uganda, Malawi, Ethiopia, Misri, Senegal, Zambia, Ghana, Malawi an Amerika.



"Tuko hapa kwa lengo la kujifunza jinzi gani shirila la PlanTanzania limeweza kupanua mtandao wake na kusaidia wajasirimali nakubadilishana mawazo ya kazi za nchi na nchi ili kuweza kusadiana kiuchumi na kuwaletea waafirika wote kipato bora kwa wnanchi hao na kutunisha mitaji yao na kuwafundisha jinsi ya kutunza fedha na kujisaidia wao wenyewe'; Alisema Muthungu.



Shirika hilo lisilo la kiserikali linalojihusisha na huduma za kijamii limeanza miradi yake kwa mara nyingine tena ili kuiwesha jamii kupata maisha bora kwa kushirikiana kwa kutoa huduma ambayo ni jnjai abora kwa maendeleo ya wananchi kuwasidia katika miradi yao mbalimbali ambapo tayari wametoa vyereani,pikipiki za miguu mitatu( Bajaj), ufugaji wenye kuleta tija, wnajifunza juu ya yan kujifunza juu ya masuala inayofanywa na ufahulu wao katika kusaidia wajasiliamli nchini Tanzania.

Alisema zaidi ya vikundi 1500 vimepata mikopo ya zaidi ya Dola za kimarekani 530,000 ili kuleta uwezo wa wananchi kwa baadae kujiendeleza kuwafundisha na kujiendeleza wenyewe kwa kubuni mradi wanaoupenda wenyewe na ambao wanaweza kuona utawapatia kipato cha haraka.

Wanachama hao kesho watakuwa katika ziara kuangalia miradi mbalimbali ya wajasiliamali jinsi gani vikundi hivyo wanajishughulisha.

MWISHO.

No comments:

Post a Comment