Friday, October 26, 2012

MAJINA YA WALIOMWUA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA YAMETAJWA NA IGP



MWANZA.

NI wiki Moja baada ya ya maziko ya yaliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP ) liberatus Barlow,Jeshi la Polisi limewataja watuhumiwa wa mauaji yake.

Kamanda Barlow aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi usiku wa kumakia Oktoba 13, mwaka huu.

Barlow  mwenye Umri wa Miaka 52 aliuawa usiku wa manane eneo la Kitangiri, Wilaya ya  Ilemela, Mkoa wa Mwanza, baada ya kutoka kwenye kikao cha harusi, alipokwenda kumshusha Mwalimu Doroth Moses, aliyekuwa amempa lifti.

Mkuu wa Jeshi la Polisi.IGP Said Mwema, akizungumza  na vyombo la habari amesema polisi inawashikilia watu 10 wakituhumiwa kuhusika na mauaji yake.

IGP  aliwataja  kuwa ni Muganyizi Peter mwenye umri wa miaka (36) aliyemkamatwa Jijini Dar es Salaam kuwa  anadaiwa  kuwa ndiye aliyempiga risasi kamanda Barlow.

Wengine waliokamatwa Jijini Dar Es Salaam  ni Chacha Mwita (50), Majinge Marwa (48), Edward Kusoka( na Bhoke Marwa (42).

 Kwa Mujibu wa IGP Mwema watuhumiwa hao walipatikana an bunduki mbili, ikiwemo Shotgun Greenner iliyokatwa kitako, inyaodaiwa ilitumika katika mauaji hayo.
Walikamatwa pia na silaha aina ya Pump Action na simu ya upepo  ya kamanda Barlow.

Amesema watuhumiwa wengine  waliokamatwa jijini Mwanza ni Mwalimu Doroth(42), Felix Felician (50), Fumo Felician (40), Bahati Lazaro (28) na Amos Bwire Bonge (30).

Kwa mujibu  wa IGP Mwema, watuhumiwa hao wapo katika mtandao wa ujambazi na wamekiri kuhusika katika matukio mengine matatu ya ujambazi Mkoani Mwanza, kabla ya wenzao kukimbilia Jijini Dar es Salaam, baada ya mauaji ya Kamanda Barlow kufanyika.

IGP SAID MWEMA, amesema kukamatwa kwa watuhumiwa  hao ni kunatokana na simu ya Mwalimu Doroth waliyokuwa wakitumia baada ya mauaji.

Watuhumiwa wawili waliokimbia Jijini Dar wanasakwa.

Hongera jeshi la polisi kwa kazi nzuri mliyoifanya, pia hongera TCRA kwa ufuatiliaji kwa njia mtandao.

Vitendo hivi vithibitiwe si kwa kamanda tu bali kwa mauji mengine ya raia pia.

Tuesday, October 23, 2012

RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA UCHAGUZI UVCCM

 DODOMA.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Jakaya Halfan Mrisho Kikwete,amefungua Mkutano wa 8 wa Jumuiya ya UVCCM Taifa huku kukiwa na taarifa kuwa mwanawe,Ridhwan Kikwete (MNEC) na  Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kudaiwa kupanga safu za uongozi.

Mkutano huo wa aina yake umefunguliwa majira ya saa 11:30,huku wajumbe wakitaka kutopangiwa safu za uongozi.

Wakizungumza kabla ya kufunguliwa kwa Mkutano huo,baadhi ya wajumbe walidai kuwa wamechoshwa kupangiwa safu za uongozi na kwamba watachagua kiongozi wanayeona anafaa na atakayekivusha chama katika harakati ya uchaguzi Mkuu wa 2015.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya kugombea Uongozi katika nafasi ya UNEC imetiafola kutokana na Kamati ya Siasa na Kamati Kuu kupendekeza majina yapatayo 40 huku vikitakiwa viti 6 (Bara),viti vinne Zanzibar wagombea wapo 22.

Kwa upande wa Baraza Kuu vijana Taifa viti vitano(Bara) wagombea wako 39 na viti vitano Zanzibar wagombea wapo 14,Uwakilishi Wazazi Taifa na UWT wagombea 16 kila nafasi.

Nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa wanaochuana ni Lulu Mushamu Abdallah, Sadifu Juma Khamis na Rashid Simai Msaraka,wakati nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Ally Salum Hapi, Paul Christina Makonda na Mboni Mohamed Mhita.

Monday, October 22, 2012

KIKWETE ALITEKELEZA ILANI KWA VITENDO.


GETI LA KUINGILIA SHULE YA KIMATAIFA ILIYOKO WILAYA YA SHINYANGA.
UWEKEZAJI KAMA HUU NDIO UNAOTAKIWA KWA NCHI YA TANZANIA ILI WATOTO WA KITANZANIA WAWEZE KUPATA ELIMU YA KIMATAIFA ILI KUKUZA UCHUMI WA NCHI YETU.















MKURUGENZI WA SHULE HIYO,FANTOM, AKISOMA HOTUBA KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, DK.JAKAYA KIKWETE MARA BAADA YA KUTEMBELEA SHULE HIYO ILIYOKO WILAYA YA SHINYANGA TANZANIA.

























NEC YA MWISHO YA MAKAMBA HII!!

ILIYOKUWA NEC YA MWISHO YA KATIBU MKUU MSTAAFU LUTENI YUSUF MAKAMBA.

WAJUMBE WA KASKAZINI PEMBA NA PWANI

WAJUMBE KUTOKA KASKAZINI PEMBA NA PWANI WAKISUBIRI UJIO WA RAIS JAKAYA KIKWETE KUWAFUNGIA KIKAO CHAO,OKTOBA 21 KATIKA UKUMBI WA JK NYERERE CHUO CHA MIPANGO DODOMA.

MAMA SOFIA SIMBA AKIPEWA ZAWADI NA MWASISI WA TANU.

MWENYEKITI WA UWT TAIFA, SOFIA SIMBA AKIPEWA ZAWADI NA WOSIA KUTOKA KWA MWENYEKITI MSTAAFU NA MWASISI WA TANU,HADIJA BINTI KAMBA (89),ANAYEISHI ILALA BUNGONI,KATIKA UKUMBI WA CHUO CHA MIPANGO DODOMA UKUMBI WA JULIUS KAMBARAGE NYERERE,AMBAPO MWASISI HUYO ALIMTAKA KUWAFUTA NA KUWAFUKUZA WANACHAMA WENYE NIDHAMU MBAYA NDANI YA CHAMA.

MUKAMA AKIMPONGEZA SOFIA SIMBA.

 KATIBU MKUU WA CCM,WILSON MUKAMA,AKIMPONGEZA KWA KUMSHIKA  MKONO MWENYEKITI WA UWT TAIFA,SOFIA SIMBA, NJE YA UKUMBI WA JK NYERERE,CHUO CHA MIPANGO DODOMA MARA BAADA YA KUTANGAZWA MSHINDI KATIKA UCHAGUZI WA UWT ULIOFANYIKA 20.10.2012

RAIS AKIWASILI UKUMBINI DODOMA.

RAIS JAKAYA KIKWETE AKIWASILI KWENYE UKUMBI WA JK NYERERE CHUO CHA MIPANGO DODOMA, KUFUNGA MKUTANO WA BARAZA LA UWT TAIFA MWENYE SUTI NYEUSI NA KATIKA NI MWENYEKITI WA UMOJA HUO,SOFIA SIMBA,PEMBENI MWA SOFIA SIMBA NI ABDULAHAM KINANA,PIUS MSEKWA NA PEMBENI MWA  JK NI KATIBU MKUU,WILSON MUKAMA.

RAIS KIKWETE ACHARUKA

DODOMA.


 MWENYEKITI WA CCM,Rais Jakaya Kikwete  amecharuka baada na kushangazwa na baadhi ya vitendo vya wajumbe vya kutaka kupigana hadharani baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa UWT uliofanyika katika  Ukumbi wa  J.K NYERERE,Chuo cha mipango.



Rais kikwete pia alionekana kukerwa na  kauli za baadhi ya wagombea kudai kuwa wanatetea kiti .

Alisema kuwa hakuna Mwenye kiti chake bali kila mwanachama anapaswa kugombea nafasi yoyote katika Chama.

Alizungumzia juu ya fujo zilizokuwa zikitaka kufanyika katika Ukumbi huo baina ya Mbunge wa Afrika Mashariki Shy-Rose Bhanji na  Sofia Simba katika Ukumbi huo alishangazwa na kitendo hicho na kwamba hakutegemea kina mama kufanya kitendo hicho cha fedheha na kinachoonyesha kutokomaa kwa wanachama wake.

'Kama wewe unajua unaweza kwa nini uweke mambo yasiyo na maana, nenda shule kasome usionee wengine,hakuna kiti cha mtu hapa kila mwanachama ana haki ya kuchukua fomu na kuomba nafasi yoyote anayoitaka kwa nini uwe na mashaka kama wewe ni mkomavu?alihoji Mwenyekiti huyo ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika ufungaji wa Baraza la UWT Taifa huku akishangiliwa na wapambe wa Anne Kilango Malecela.


Mara baada ya hotuba kali ya RAIS wapambe wa ANNE KILANGO MALECELA walionekana kufurahi huku kila mmoja kipiga simu mikoani na kusema kuwa 'kwa kweli tuna amani kubwa, RAIS amezungumza,amesema sana,kwa kweli hotuba hii ingekuja jana,tungeshinda katika uchaguzi huu,alisikika Mjumbe Mmoja akizungumza na wana UWT kwa njia ya simu.


JK aliendelea kusema Chama kinapokwenda sipo,kama unataka madaraka kwa rushwa wewe si kiongozi,UWT ni jeshi kubwa,na Maana yake ni kuhakikisha chaguzi zinafanyika kwa huru na haki pia   maana ya UWT na Kwa mujibu wa katiba ya TANU akinukuu alisema Dhana ya TANU ni kuhakiksiha Chama kinashinda katika chaguzi zote kuanzia Kitongoji,hadi Taifa na lazima tuangalie 2015 Kinashika dola kuanzia nafasi zote.

'Ni vitu vya ajabu sana vinafanyika kwa upande wa NEC walikuwa wamekata majina ya watu, kwa nini uwakata waache wakashinde wenyewe ukumbini , mkifanya hivi kutakuwa na hatari mbele ya safari,watasema aah!!! Chama kina wenyewe....wenyewe yeye atakuwa hayumo ni hatari sana! alisema JK.

Mara baada ya hotuba hiyo, Rais Kikwete aliwakaribisha wajumbe hao kupata chakula cha Usiku na kuagana nao kwa kuwatakia safari njema na kufanya kazi kwa bidii ili CCM iendelee kuongoza dola.

Wajumbe hao wameondoka leo alfajiri kuelekea Mikoani,huku nyumba za kulala wageni zikipokea wajumbe VIJANA,na maisha yakiendelea kuwa magumu kutokana na uhada wa chakula,kupanda bei kwa baadhi aya vyakula na hivyo kufanya wakazi wa Mjini Dodoma kuambulia mboga za majani na nyama ikiwa 

Amewataka walioshindwa katika nyandifa za UNEC  wa Wilaya kupitia CCM wawe na subra, na kwamba waendelee kukitumika Chama kwa nguvu zao zote bila kujali.

Umoja wa Vijana kesho utafanya Chaguzi zake kwa nafasi mbalimbali za uongozi, huku wajumbe kutoka Mikoa mbalimbali wakiwasili.


Wajumbe kutoka Mkoa wa Mara, Kigoma na Mbeya tayari wameishawasili na maandalizi ya malazi yameifanyika,huku shamra shamra kutoka bendi ya Vijana jazz ikitumbuiza katika Makao Makuu ya Chama Mjini Dodoma ambapo pia ni Makao Makuu ya Tanzania.



MLEMAVU WA NGOZI AJITOSA NEC VIJANA



DODOMA.

Mlemavu wa  Ngozi Fatma Jumbe Mwalimu amejitokeza kugombea Ujumbe NEC viti 6  na Baraza kuu Taifa viti vitano Bara


Akiwa katika ofisi za Makao Makuu ya Chama Mjini Dodoma alipokuwa akijinadi kwa wapiga kura kutoka Mkoa wa Mara,Mbeya na Kigoma mara walipowasili kutoka Mikoa hiyo 

Alisema kuwa atasimamia maslahi ya vijana kwenye vikao husika,kuipa UVCCM nguvu ya kiuchumi na kimaamuzi na kuimarisha jumuiya na kuhakikisha ushindi wa kishindo ifikapo 2015 katika uchaguzi Mkuu.


Fatma ameongeza kuwa vijana ndiyo nguvu ya Chama na kwamba na kwamba msingi wa maendeleo ya vijana ni vijana wenyewe.

Katika uzoefu ndani ya Chama ni Mjumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM UDSM,Mjumbe Baraza la vijana Mkoa wa Ruvuma, Mjumbe Baraza la UWT Mkoa wa Ruvuma, Katibu Mkuu Jumuiya ya walemavu UDSM (DUAH),Naibu Waziri Maji na Mazingira UDSM, na Afisa afya na mazingira kata ya Ubungo.


Kwa upande wa elimu ana Shahada ya ualimu aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na sasa ni Mwalimu shule ya Sekondari ya wasichana Songea.

Wengine waliokuwa wanajinadi na kutoa vipeperushi vyao ni Beatrice Omolo anayegombea NEC, Nadra Rashid NEC,Edna Kwilasa NEC nafasi 6 Bara,Fadhila Nassor Abdi NEC viti 4 Sango Kasera NEC Zanzibar,Lulu Abdallah NEC viti 4 Zanzibar,Neema Nyangalilo Mgombea NEC,Anthony Mavunde mgombea NEC,Jerry Silaa Mgombea NEC Hassan Chamshama NEC viti sita Bara,Neema Mwandabila NEC nafasi 6 Bara
Esther Sato Makune na Zainabu Katimba wanaogombea Baraza Kuu Taifa nafasi tano,


Wengine niliopata nafasi ya  kuzungumza nao  na kwamba wako imara na kuhakikisha Chama kinaendelea kushika dola ni Mwanawewe Ussi Yahaya anayegombea  BarazaKuu Taifa nafasi tano Zanzibar ,Rashid Gewa  na Asha Abdalla anayegombea Nafasi ya Halmashauri Kuu kupitia UVCCM viti vinne Zanzibar.


Aidha vijana Makao Makuu hapa Dodoma wamepamba Moto zaidi kwa Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Paul Makonda ambapo baadhi ya wajumbe wamekuwa wakibeba bago lako likiwa na maandishi ya heshima, uwezo na utu wa mgombea upimwe kwa mchango wake katika jamii wala sio kundi au fedha alizonazo.

Monday, October 15, 2012

HOTEL ALIYOIPENDA MAREHEMU KAMANDA BARLOW

GOLD CREST HOTEL YA JIJINI Mwanza, ambapo Marehemu alipenda kupumzika na kufanya mazungumzo pia  Chakula cha Usiku.

ROUND ABOUT ya NYERERE Inayoungana na Kenyata na kuelekea Uwanja wa Ndege wa Mwanza iliyokuwa ikitumiwa na Kamanda Barlow katika Shughuli mbalimbali za Ulinzi wa Amani Mkoani ambapo ni Mita chache kutoka ofisini kwake, Mkabala na Bandari ya North Port.

KAMANDA LIBERATUS BARLOW AAGWA MWANZA.




KAMANDA W A POLISI MKOA WA MWANZA,KAMISHINA MSAIDIZI  (ACP)  LIBERATUS BARLOW ANAAGWA LEO KATIKA VIWANJA VYA NYAMAGANA JIJINI MWANZA.


ACP BARLOW aliua usiku wa kuamkia oktoba 13 maeneo ya kitangiri na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi akitoka kumshindikiza mwanamke mmoja,Mwalimu wa Shule ya msingi Nyamagana aliyejulikana moja la Doroth Isasia Moses.

Kwa mara ya kwanza kutokea  nchini Tanzania kufanyika mauaji ya Kamanda wa Polisi.

Hii ni mara ya Kwanza kwa nchi yetu yenye UPENDO,AMANI na UTULIVU kupatwa na simanzi na majonzi kwa mauji ya kikatili kwa kiongozi wa ngazi ya juu, nchini Tanzania.

Mimi Eva-Sweet Musiba,nimesikitishwa sana na taarifa hizi za mauaji ya Kamanda na nimepata simanzi kubwa kwa upande wangu na machozi yanatiririka  kila wakati nabaki kujiuliza tunakwenda wapi na tumetoka wapi.
Dhana na polisi jamii iangaliwe kwa makini sana, nadhani Kamanda Barlow alichukulia watu hao kuwa wana 

Amani kumbe sivyo ndivyo, alijua kuwa ni wenzake kumbe la!

Naomba jeshi la polisi kuwa makini sana,kwani kuna baadhi ya askari hata Bastola hawana wakiwa katika doria.
Mh.Emmanuel Nchimbi,Waziri wa Mambo ya ndani, pole kwa kupatwa na msiba mkubwa,jipange vyema ili kuboresha maisha ya askari wetu ambao wafanya kazi kubwa na hatari sana katika maisha yao.

Natoa pole kwa familia ya marehemu,Wakazi wa Jiji la Mwanza, Arusha na Watanzani wote kwa ujumla.

Baada ya mwili huo kuagwa Jijini Mwanza utasafirishwa kuelekea Jijini Dar Es Salaam eneo la Ukonga nyumbani kwa marehemu ambapo utaagwa na kuzikwa Oktoba 17  nyumbani kwao Marangu Moshi. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz pokea kamanda na mpiganaji mwenzio.


KAMANDA WA POLISI MKOA WA KILIMANJARO,ROBERT BOAZ